Jiongeze: Aziz Ki kabeba pesa na dada yetu
Muktasari:
- Inaumiza sana. Amebeba pesa zetu na dada yetu. Kaondoka zake kafuata pesa za Waarabu Morocco. Kina Fei Toto wapo hapa hapa. ‘Wai’ Fei?
Dar es Salaam. Alichukuliwa kutoka Ivory Coast na kuletwa Tanzania. Alichotakiwa kufanya kakifanya, kisha kaenda zake Morocco. Akiwa mbali alionekana yeye. Akiwa karibu kaonekana yeye tena.
Inaumiza sana. Amebeba pesa zetu na dada yetu. Kaondoka zake kafuata pesa za Waarabu Morocco. Kina Fei Toto wapo hapa hapa. ‘Wai’ Fei?
Yes! Ndiye mkali wetu. Ndiye tegemeo letu ndani ya ligi kuu. Wapo wengi ila Fei ni mzawa sahihi anayesimama daraja moja. Na wageni katika eneo la kiungo na anayefunika.
Aziz kaja, Fei hana wazo la kuondoka. Aziz kaondoka Fei hana ndoto wala mipango ya kuondoka nchi hii.
Huhitaji maneno ya Nabii na Mtume. Ili ujue Fei hana mpango wa kutoka. Mpaka sasa tetesi juu yake ni Simba na Yanga tu. Mara chache tumesikia Nabi akimtaka Kazier. Lakini tetesi za Jangwani na Msimbazi, zinaonekana usahihi zaidi.
Lini ulisikia Aziz Ki kutoka Yanga na kwenda Simba? Ni kwamba Aziz Ki alihusishwa na nje ya Bongo zaidi. Na ndicho kilichotokea kasepa. Mwanaye Fei huenda msimu ujao akawa Yanga au Simba. Inaumiza!
Emmanuel Amunike. Mosi ni kocha. Pili mzaliwa wa Nigeria, tatu kacheza soka la Ulaya, nne alikuwepo kwenye kikosi bora cha Nigeria cha 1996. Na zaidi amechezea Barcelona. Mwenye sivii kubwa hivyo. Akiwa kocha Stars. Kwa mdomo wake, alisema Fei Toto anacheza timu yoyote Ulaya.
Unataka nani akuambie ubora wa Fei zaidi yake? Mayele kaja kaondoka. Chama kaja kaondoka karudi. Inonga kaja na kusepa. Fei bado yupo akiwa na ubora ule ule. Achana na hao. Aziz naye? Fei kwanini aendelee kulipwa na kina Sopu, Nkane na Andambwile? Kususa mechi za mwisho kwa Yanga lilikuwa kosa kubwa.
Ule ndo ulikuwa wakati sahihi wa kujiuza. Angecheza fainali ya shirikisho, stori zingekuwa tofuati. Fainali ya shirikisho ilimuuza Mayele. Imemuuza Aziz Ki. Bila shaka kabla ya Aziz Ki tungeuza Fei Toto.