Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utitiri wa tozo watajwa kikwazo kuvusha bidhaa Zanzibar kwenda Bara

Muktasari:

  • Utaratibu wa tozo na ushuru kuvusha bidhaa kutoka Zanzibar kwenda Tanzania bara, umetajwa kuwa kikwazo cha ukuaji wa viwanda.

Dar es Salaam. Wingi wa tozo, ushuru na kodi katika mchakato wa kuvusha bidhaa kutoka Zanzibar kuingia Tanzania Bara, umetajwa kuwa kikwazo cha maendeleo ya viwanda visiwani humo.

Kulingana na Chemba ya Biashara Zanzibar, bidhaa zinazotoka visiwani humo zinatozwa kodi kubwa ya kuziingiza bara, ilhali yote ni nchi moja.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo, Septemba 22, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara Zanzibar, Hamad Hamad aliposhiriki kikao kazi kuhusu changamoto za biashara za mipakani kilichoandaliwa na Liberty Sparks.

Hamad amesema haikupaswa kuwepo na ushuru wa kuvusha bidhaa hizo kutoka Zanzibar kuingia bara ilihali ni taifa moja.

"Ilipaswa wafanyabiashara walipie ushuru wa bandari tu, kwa kuwa wanasafirisha kupitia bandarini lakini hakukupaswa kuwepo tozo nyingine utadhani unasafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine," amesema.

Utaratibu huo, amesema unasababisha wafanyabiashara kutoka Zanzibar kukumbana na kodi kubwa.

"Sisi kule Zanzibar tuna viwanda na soko letu ni Bara, maana idadi ya watu kule ni ndogo, lakini kuvusha biashara ni changamoto na ndiyo sababu ya viwanda vya Zanzibar kukosa masoko," amesema.

Mkurugenzi wa Liberty Sparks, Evance Exaud amesema kulingana na ripoti yao ya mwaka jana mwenendo wa biashara za mipakani ni asilimia 6.02.

Amesema kiwango hicho ni kidogo kutokana na mazingira magumu yaliyopo na kwamba kunahitajika juhudi za makusudi kutatua hilo.

Kulingana na Exaud, kampeni ya ujirani mwema unalenga kuboresha mazingira ya biashara za mipakani ndiyo utakaokuwa suluhu ya changamoto hiyo.

"Tunachokifanya ni kushirikisha wadau tujadili mbinu za kutatua changamoto zilizopo ili angalau tufikie asilimia nane katika biashara za mipakani na tuwe na mazingira mazuri zaidi ifikapo mwaka 2032.