Rais Mwinyi ataka mabalozi kutangaza uchumi wa buluu

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema Zanzibar bado ina mahitaji makubwa ya uwekezaji kwenye sekta ya uchumi wa buluu kupitia utalii, uvuvi na ufugaji wa vifaranga vya samaki hivyo kuwataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa ya nje kuyatangaza maeneo hayo.
Maeneo mengine ambayo bado yanahitaji uwekezaji ni bandari, mafuta na gesi na sekta ya usafirishaji wa majini.
Dk Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na mabalozi wateule waliofika kujitambulisha, kupokea nasaha pamoja na kuaga kuelekea vituo vyao vya kazi kwenda kuiwakilisha Tanzania Kimataifa.
Dk Mwinyi aliwasishi mabalozi hao kuzichangamkia fursa za uwekezaji huko kwenye vituo vyao vya kazi na kuzileta nchini ili kuiimarisha utalii wa Zanzibar ambao nitegemeo kwa uchumi wa nchi unaochangia asilimia 30 ya pato la taifa.
“Bado inahitaji kuwkza zaidi katika maeneo hayo kwahiyo mnapokwenda huko kuiwakilisha Tanzania kimataifa, hakikisha mnayatangaza vyema maeneo hayo ili waje Zanzibar kuwekeza,” alisema
Aliwataka mabalozi hao kuangalia zaidi soko jipya la utalii mbali na kutangaza utalii wa fukwe na urithi lakini pia kuangalia fursa mpya za utalii wa mikutano, michezo na uwekezaji ili kuitangaza zaidi Zanzibar.
Kuhusu sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki, Dk Mwinyi aliwataka mabalozi hao kuitangaza zaidi fursa hiyo pamoja na kutafuta wawekezaji na masoko ya kilimo cha mwani ambapo Zanzibar inaongoza kwa kuzalisha mwani Afrika.
Alisema Zanzibar inahitaji Bandari kubwa jumuishi ili kukidhi mahitaji ya uchumi wake kama kituo muhimu cha usafirishaji, usambazaji wa bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Kwa upande wa mafuta na gesi na mafuta na gesi, Mkuu huyo wanchi alisema Dk Mwinyi alisema Zanzibar inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sekta hizo ili kuimarisha sekta ya biashara na uchumi wake kupitia bandari za Zanzibar, Tanga, Dar es Salaam, Mtwata, Msumbiji na Komoro.
“Zanzibar inahitaji vyombo vya usafiri wa majini kwa safari za Pemba, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na kwengineko kama Msumbiji, Komoro na sehemu nyingine za visiwa zilizozungukwa na bahari,” alisema
Kwa upande wao mabalozi hao walimuhakikishia Rais Dk Mwinyi kuzifanyia kazi nasaha na maelekezo aliyowapa wakati wote wa utumishi wao na kumuahidi kuchangamkia vyema fursa zilizomo kwenye maeneo yao ya kazi kwa lengo la kuendelea kuiimarisha Diplomasia ya Uchumi na kuiendeleza kwa vitendo Sera ya Uchumi wa Buluu.
Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake, Balozi Khamis Mussa Omar anayekwenda kuiwakilisha Tanzania jijini Beijing, China alisema watahakikisha wanatekeleza maagizo hayo kwa uaminifu.
Pia alisema watakwenda kuboresha zaidi uhusiano na ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na mataifa hayo pia kuimarisha ujirani mwema wa mabalozi wa vituo vilivyopo kwenye nchi jirani kwa kuhakikisha wanasimamia usalama wa nchi na kukuza uchumi na biashara baina yao.
Mabalozi wengine ni Balozi Hassan Mwamweta anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Ujerumani na mataifa ya Bulgaria, Czech, Hungary, Old Swiss, Poland, Slovakia na Switzerland.
Wengine ni Balozi, Habibu Awesu Muhamed anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Qatar, Balozi Mohamed Juma Saudi Arabia, Imani Njikai Algeria, Balozi Meja Jenerali Ramson Mwaisaka atakaeiwakilisha Tanzania nchini Misri, Balozi Gelasuis Byakanwa ataiwakilisha Tanzania nchini Burundi na Balozi Dk. Benard Kibesse ataiwakilisha Tanzania jijini Nairobi, Kenya
Mabalozi hao wanane waliapishwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Agosti 16 mwaka huu baada ya kuwateua kushika nafasi hizo Mei mwaka huu.