Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa Makame: Wanasiasa mna nafasi kubwa kwenye maridhiano

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (Suza), Profesa Mohamed Makame Haji.

Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (Suza), Profesa Mohamed Makame Haji amechambua 4R za Rais Samia Suluhu Hassan huku akisisitiza umuhimu wa maridhiano na nafasi ya wanasiasa katika jambo hilo.

Profesa Makame amebainisha hayo leo Septemba 13, 2023 wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa wadau wa demokrasia kujadili utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi.

Profesa Makame Haji ameeleza historia ya siasa za Tanzania kabla, wakati na baada ya uhuru pamoja na kuchambua 4R za Rais Samia na umuhimu wake katika ujenzi wa Taifa.

Amesema wanasiasa wana nafasi kubwa katika maridhiano kwa sababu wana ushawishi mkubwa katika jamii na wengine ni wawakilishi wa wananchi.

"Mwaka 2010, Zanzibar ilifanya marekebisho ya Katiba na kuja na wazo la kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Maridhiano ya aina hii na mengine yatakayofuata, ndiyo yanayotakiwa katika kuendesha nchi hii," amesema Profesa Makame.

Kuhusu mageuzi, mwanazuoni huyo amesema yanahitajika leo ma siyo kesho na mageuzi hayo yahusishe mabadiliko ya sheria na Katiba.

"Lazima tusimame kuhakikisha mageuzi yanaletwa kwa manufaa ya Watanzania wote na kuwawezesha kunufaika na rasilimali zao," amesema Profesa Makame wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.

Vilevile, amezungumzia ujenzi wa Taifa akisema ujenzi huo utatokana na Taasisi zinazosimamia mageuzi. Amesisitiza kwamba Tanzania wanayoitaka ni ile inayozingatia maslahi ya wananchi.