Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Othman: Tunakwenda kuzisemea changamoto za Watanzania

Muktasari:

  • Othman ambaye ni Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, amesema mkutano mkuu huo maalumu unakwenda kuweka utaratibu na miundombinu itakayowakwamua Watanzania pale walipokwama.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema mkutano mkuu wa maalumu wa chama hicho, unakwenda kutengeneza ramani ya kuwapatia Watanzania watu watakaozisemea changamoto zinazowakabili.

Mbali na hilo, Othman ambaye ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema mkutano mkuu huo maalumu unakwenda kuweka utaratibu na miundombinu itakayowakwamua Watanzania pale walipokwama.

Othman ameeleza hayo leo Jumatano Agosti 6, 2025 wakati akielezea madhumuni ya mkutano mkuu wa maalumu unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambao hadi mchana wajumbe 634 kati ya 736 walijisajili.

"Mkutano mkuu unakwenda kupaza sauti za Watanzania ambazo zimezimwa na kuzuia kwa muda mrefu. Mkutano huu unakwenda kutengeneza ramani na miundombinu ya kuwapatia Watanzania watu watakaosemea changamoto zao pale ambapo wamekwama," amesema.

"Njia ya sauti zao kusikika ni kuweka viongozi wanaowataka na kuwa na uwezo wa kuwawajibisha. Mkutano huu unakwenda kuwatoa Watanzania huko waliko, naomba tusiwaangushe wananchi," amesema Othman.

Othman ambaye anawania urais wa Zanzibar kwa mara ya kwanza amefafanua ACT Wazalendo kinakwenda kwenye mapambano ambayo silaha ya mwanzo ya mwanajeshi yeyote si bunduki wala mzinga bali nidhamu.

"Niwaombe wajumbe mkutano mkuu kusimamia masilahi ya Watanzania kwa nidhamu ili tufanikiwe. Tumeamua kuwatumikia Watanzania lakini tubaki kwenye nidhamu," amesema Othman.


Ofisi ya Msajili

Awali, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema ofisi hiyo inawapongeza ACT Wazalendo, kwa kufanya mkutano mkuu huo ambapo wamekamilisha takwa la kidemokrasia.

Nyahoza ambaye alikuwa anamwakilisha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema jukumu la ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ni kufuatilia vyama vya siasa kuhakikisha vinafuata sheria.

"Tunakwenda kwenye uchaguzi kuna vyama vya siasa, hivyo tunavipongeza na kiviasa vizingatie sheria na kufuata utaratibu uliowekwa ili kudumisha amani," amesema Nyahoza.


Asasi za kiraia

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa amewapongeza ACT Wazalendo kwa kuendelea kutambua asasi za kiraia kwenye suala la demokraaia na utawala bora.

"ACT Wazalendo walitupa nafasi ya kuwasilisha maoni yetu, tunaamini ilani itakayozinduliwa leo itabeba yale maono tulioyawasilisha tulipoitwa, ikiwemo Katiba Mpya," amesema Ole Ngurumwa.

Ole Ngurumwa amesema vyama vya siasa ndio mlango pekee wa kutimiza ndoto za Watanzania ili kushiriki nafasi za uongozi kwa ngazi mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Ole Ngurumwa amesema kuelekea uchaguzi kila chama kina mpango mkakati ikiwamo kuja na  kaulimbiu 'Oktoba tunatiki' kingine Oktoba Linda Kura' na wengine No reforms no election.'

"Kikubwa tusibezane kila mtu anayeamini njia yake basi aachwe kwa sababu kila chama nia yake ni kuchukua dola. Chama vinavyotaka kuchukua dola vihakikishe vinakuwa pamoja hasa katika ushirikiano," amesema Ole Ngurumwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (Wildaf), Anna Kulaya amesema; "Tunashukuru kuwa sehemu ya kushiriki mkutano mkuu maalumu tunawapongeza ACT Wazalendo kwa maandalizi mazuri.