Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgombea urais NRA achukua fomu, ataja mambo matatu muhimu

Muktasari:

Katika msafara huo, mgombea aliongozana na watu wengine waliokuwa kwenye magari madogo matatu yaliyofungwa bendera za chama hicho.

Dodoma. Mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Almasi na mgombea mwenza, Hamis Hassan Majukumu wamefika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea.

Wawili hao wamefika katika Ofisi za INEC mtaa wa Njedengwa saa 7:55 mchana na kupokelewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ramadhan Kailima.

Katika msafara huo, waliongozana na watu wengine waliokuwa kwenye magari madogo matatu yaliyofungwa bendera za chama hicho.

Wengine walikuwa waendesha pikipiki ambao nao walifunga bandera kubwa kwenye viti vya nyuma katika vyombo vyao.

Tofauti na mgombea wa CCM, msafara wa NRA umeruhusiwa kuingia ndani moja kwa moja na vyombo vyao hadi lilipo lango la kuingia ndani ya ukumbi wa INEC.

Hata hivyo, CCM walikuja na matarumbeta na kikundi cha mdundiko wakati NRA wao hawakuwa na kelele zaidi ya msafara wao kutawaliwa na milio ya pikipiki na magari bila kelele.

“Ndugu mgombea, hapa ndiyo Ofisi za Tume, karibu ndani, kwa utaratibu wetu utakaa mahali kisha utatupa barua zao tuzipitie kujua uhalali wako kisha tutafuata taratibu zingine,” amesema Kailima akimweleza Almasi.

Mara baada ya maelekezo hayo, Kailima ameongozana na wagombea hao kuingia ndani ya jengo na wapambe wachache waliokuwa wamewasindikiza.

Mgombea huyo ametumia dakika 22 kisha akatoka na akazungumza kwa kifupi na vyombo vya habari.

Akizungumza nje ya lango, Almasi amesema wanaamini ushindi wao ni katika mambo matatu.

“Hatua hii tumemaliza, kinachofuata ni mambo matatu; kwanza, Mungu, wapigakura na baadaye Tume kututangaza, kinyume na hapo lazima Taifa kwanza,” amesema Almasi.

Mgombea huyo ameeleza kuwa NRA wako tayari kukosa uongozi lakini nchi ibaki salama kuliko kukimbilia uongozi wakati wakigundua Watanzania hawajawachagua na kusababisha nchi ikose usalama.