Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchakato kuwapata watiania udiwani, ubunge ACT Wazalendo waiva

Muktasari:

  • Akitoa salamu fupi za chama, Ado amewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa maalumu akisema ACT Wazalendo inawatiania wa udiwani katika kata zote za Tanzania Bara na Zanzibar akisema ndio silaha za kuiondoa CCM madarakani.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema chama hicho kimekamilisha mchakato wa kuwapata watiania wa udiwani, uwakilishi na ubunge kwa Tanzania Bara na Zanzibar, akikitaka Chama cha Mapiduzi (CCM) kijiandae.

Katika ukamilishaji wa mchakato huo, Ado amesema kumekuwa na maombi mengi ya makada wa vyama mbalimbali wanaotaka kujiunga na ACT Wazalendo, akisema milango ipo wazi ili kuunganisha nguvu ya kuiondoa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Jumatano, Oktoba 29, 2025.

Ado ameeleza hayo leo Jumatano Agosti 6, 2025 wakati akielezea madhumuni ya mkutano mkuu maalumu unaondelea katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akitoa salamu fupi za chama, Ado amewaambia wajumbe wa mkutano huo ACT Wazalendo ina watiania wa udiwani katika kata zote za Tanzania Bara na Zanzibar akisema ndio silaha za kuiondoa CCM madarakani.

"Pia tumeshakamilisha mchakato wa kuwapa watiania ubunge na uwakilishi wa Zanzibar, vivyo hiyo katika majimbo ya Tanzania bara CCM ijiandae," amesema Ado.

Mbali na hilo, Ado ambaye ni mtiania ubunge wa Tunduri Kusini mkoani Ruvuma amebainisha kuna vuguvugu na wimbi kubwa la watu wanaobisha hodi kutaka kuingia ACT Wazalendo ili kuunganisha nguvu za kuindoa CCM.

"Njooni tuunganishe nguvu ya kuiondoa CCM madarakani," amesisitiza Ado.

Kuhusu mkutano mkuu maalumu, Ado amesema:"Tumekutana hapa ili kuhitimisha mchaktao wa juu wa kuandaa watiania wa urais wa Tanzania na Zanzibar, lakini pia kuhitimisha safari ya ilani ya uchaguzi mkuu. Lakini mwisho tutajipanga kwa ajili ya mipango ya ushindi wa uchaguzi.”

"Bahati nzuri ACT Wazalendo kimekuwa kiongozi kwenye yote hasa kuandaa wagombea kuanzia udiwani hadi urais. Tangu mwaka 2015 ACT Wazalendo kimekuwa kikiandaa ilani bora tena kimekuwa hodari kuandaa mipango kabambe ya uchaguzi," amesema Ado.


Endelea kufuatilia Mwananchi