Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Devota:Chagueni Chaumma chakula kishuke bei, vijana wawe na uhakika wa ajira

Mgombea mwenza wa urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devota Minja

Muktasari:

Chama hicho kimesema, endapo kitashika madaraka na kuunda Serikali mchele utashuka bei hadi Sh500 kwa kilo pamoja na utitiri wa ajira.

Arusha. Mgombea mwenza wa urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devota Minja ameshangazwa na ugumu wa maisha walionao Watanzania wakati nchi imebarikiwa kila kitu.

Amesema haiwezekani baadhi ya watu wakose hata buku (Sh1,000) mfukoni, mchele kilo Sh3,000 huku   wengine hata chai hawanywi asubuhi kutokana na kukosa pesa.

Akihutubia leo Jumatatu Septemba 22, 2025 aliposimama njiani Usa River Jimbo la Arumeru Mashariki akiwa njiani kuelekea Moshi,  Minja amesema serikali ya Chaumma itatengeneza mazingira ya upatikanaji wa chakula kirahisi pamoja na ajira za kutosha.

"Mchele utashuka bei hadi Sh500 ajira za kutosha zitokanazo na utalii hapa Arusha, ardhi watapewa watu walime. Haiwezekani watu wawe na maisha magumu wakati nchi ina utajiri na fursa," amesema na kuongea:

"Mungu ametupatia kila neema, bahari, maziwa, mito, ardhi, madini ya kila namna, vivutio vya utalii, yote haya CCM imekosea mikakati tupeni Chaumma tuje na mikakati mizuri," amesema.

Akieleza sekta ya kilimo amesema ardhi iliyopo itawezesha kilimo cha kimkakati, kutakuwa na viwanda vya mbolea, viatilifu na dawa ili watu walime, chakula kiwe cha kutosha kishuke bei.

Amesema lengo la hayo yote ni kuhakikisha Watanzania hawana njaa. Mikakati yao ni kutoa matrekta, pamoja na zana zote za kilimo kwa urahisi.

"Tunataka watu wawe na chakula kila wilaya kuwe na akiba, watu wapate chakula hata wakienda hospitali kutibiwa wapate chakula.

"Mchele utauzwa Sh500 kutokana na kuondolewa kwa gharama za uzalishaji wa chakula. Watu wakiwa na uhakika wa chakula watafanya vitu vingine vya maendeleo," amesisitiza.

"Tutaenda nao bampa tu pampa hadi kieleweke, lazima CCM tuitoe madarakani hivyo watu tukapige kura tuchague Chaumma," amesema.

Akiambatana na mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Jackline Kimambo, ambaye amesema wana Arusha wakimpa ridhaa ataondoa ushuru wa soko jimboni humo.

"Huku tupo karibu na mlima Meru lakini watu tunakunywa maji yenye magadi, haiwezekani, kuna vijana bodaboda lakini ni wasomi wanachomwa na jua," amesema.

Amesema endapo akiingia bungeni ataenda kuwasemea watu wote hao pamoja na matatizo waliyonayo.

Chaumma inaahidi hayo wakati kampeni za uraisi, wabunge na madiwani zinaendelea kuchanja mbuga kote nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.