Tanzania imepiga hatua katika kuendeleza hifadhi na maeneo tengefu ya bahari
Muktasari:
Mara nyingi watu wanaposikia neno hifadhi mawazo yao moja kwa moja hukimbilia kwenye hifadhi za taifa zilizopo nchi kavu kama vile Mbuga za Wanyama za Serengeti, Ngorongoro, Mikumi na nyinginezo, lakini ni nadra mno kusikia watu wakitaja hifadhi zinazopatikana katika bahari.
Wakati hali ikionyesha hifadhi za bahari kutokuwepo akilini na midomoni mwa watu wengi, Tanzania inajulikana kuwa miongoni mwa mataifa duniani ambayo yamejizolea sifa kubwa katika kusimamia vizuri hifadhi za bahari.
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ni nini?
Kwa mujibu wa Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dkt. Adilian Chande, kitengo hicho kilikuwa chini ya Idara ya Uvuvi, kwa mujibu wa sheria ya Maeneo Tengefu ya Bahari Na. 29 ya mwaka 1994.
Kutokana na kwamba kwa sasa Sekta ya Uvuvi imegawanyika katika idara mbili; Ufugaji wa Samaki na Maendeleo ya Uvuvi, kitengo sasa kipo chini ya Idara ya Maendeleo ya Uvuvi.
"Hivyo sheria iliyounda kitengo kwa sasa ipo redundant (imepitwa na wakati), kwani idara ya Maendeleo ya Uvuvi haijatajwa kwenye sheria ya wakati huo na sasa tupo katika mchakato wa kurekebisha sheria," alisema Dkt. Chande.
Akizungumza mwaka jana wakati wa kupokea ujumbe wa watendaji wa Mradi wa Kuhifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP) uliokuwa kwenye ziara ya kujifunza kutoka kwenye miradi inayotekelezwa kuhifadhi mazingira ya Ukanda wa Pwani na hasa Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingira ya Ukanda wa Pwani (TCMP) unaofadhiliwa na USAID, Dkt. Chande alisema kitengo kilianzishwa baada ya idara kugundua kuwa kulikuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hasa katika maeneo yenye bayoanuai kubwa na viumbe ambao ni adimu baharini kama vile nguva, pomboo, kasa, papa na wengine ikiwa ni pamoja na uoto wa asili ambapo mikoko ilikatwa ovyo na matumbawe kuharibiwa kwa kupigwa mabomu.
"Matumbawe yalivunjwa ovyo ovyo kwa kutumia mabomu, shida kubwa ni mabomu ambayo yanaangamiza matumbawe ambayo ndiyo uhai wa bahari, hakuna bahari bila matumbawe, hakuna uhai kabisa," alisema Dkt. Chande.
Ndipo idara ikaona kuna haja ya kuanzisha kitengo kuweza kubainisha maeneo husika ili yaweze kuhifadhiwa kwa njia mbili, Hifadhi za Bahari au Maeneo Tengefu.
Kwa kutofautisha, Hifadhi ya Bahari ni eneo kubwa ambalo hata watu wanaishi ndani yake. Shughuli za eneo hilo husimamiwa na Mpango wa Usimamiaji ujulikanao kama General Management Plan, ambao kwa mujibu wa Dkt. Chande, maandalizi yake yanashirikisha wadau wote.
Mpango unashirikisha wanajamii ambao wanaishi ndani ya hifadhi, Halmashauri husika ambazo ziko ndani ya hifadhi, na wadau wengine ikiwa ni pamoja na wanasayansi kwa kushirikiana na uongozi wa kitengo kukubaliana kuwa baadhi ya maeneo yatengwe kabisa ambapo hakuna uvuvi wowote utakaoruhusiwa, kutenga maeneo ya matumizi ya jumla ambapo uvuvi unaruhusiwa kwa wavuvi wa ndani na nje ya hifadhi na maeneo ya matumizi maalum ambayo pamoja na kwamba wavuvi wa ndani ya hifadhi wanaruhusiwa kuvua kwa kutumia zana maalum zinazoruhusiwa kisheria, wavuvi wa nje hawaruhusiwi kabisa kuvua katika maeneo hayo.
Kwa upande mwingine, maeneo tengefu ni maeneo madogo madogo ya visiwa ambayo yanazungukwa na matumbawe. Katika maeneo haya watu hawaruhusiwi kuishi wala matumizi ya rasilimali hayaruhusiwi. Shughuli zinazoruhusiwa katika maeneo hayo ni zile zinazohusiana na utalii tu. Kwa mujibu wa Dkt. Chande, maeneo hayo ni pamoja na visiwa vya Bongoyo na Mbudya mjini Dar es Salaam ambapo ndani yake kitengo kimetengeneza njia vinjari (nature trails) kwa ajili ya watalii kupita.
Je, Unazijua Hifadhi za Bahari Tanzania?
Kwa mujibu wa Dkt. Chande, ni mpango wa dunia nzima kuwa asilimia 10 ya maji ya bahari na maziwa yanakuwa chini ya hifadhi, na Tanzania ina asilimia 4.5 tu ya hifadhi. Alisema kama kitengo chake kitaingia katika kuanzisha hifadhi kwenye maji ya ziwa, anatarajia asilimia hiyo itaongezeka hadi 7 na hivyo nchi kupiga hatua kubwa.
Asilimia hiyo 4.5 inahusisha hifadhi za bahari 3 na maeneo tengefu 15. "Tuna Hifadhi za Bahari 3 nchini Tanzania," alisema Dkt. Chande.
Akizitaja kwa majina, alisema hifadhi ya kwanza ni ile ya kisiwa cha Mafia katika Mkoa wa Pwani ambayo ilianzishwa kati ya mwaka 1995/96. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mraba 822.
"Katika hifadhi hii huwezi kusikia bomu linalia kwani tumeshadhibiti hali na wananchi wengi wameshakuwa na uelewa na hivyo kusaidia katika kazi za uhifadhi," alisema na kuongeza kuwa pia wananchi wanafaidika kutokana na kuongezeka kwa utalii katika eneo hilo.
"Kuna geti la kuingilia kwenye hifadhi na kiingilio ni dola 20. Kila mwaka wanakijiji wanapata asilimia 20 na halmashauri asilimia 10 ya mapato yatokanayo na utalii," alibainisha na kuongeza kuwa kila mwaka wanakijiji wanaandaa mpango wao wa shughuli za maendeleo ambao unapitishwa na halmashauri husika. Mpango huo unabainisha vijiji vya kufaidika na fedha za hifadhi mwaka hadi mwaka na unaweza kuhusisha shughuli za uchimbaji visima, kujenga zahanati, madarasa na shughuli nyingine.
Pia, kitengo hicho kinasomesha baadhi ya watoto wa wanajamii katika hifadhi katika kiwango cha elimu ya sekondari ili kuhamasisha jamii hizo kupenda kupeleka watoto wao shule.
"Kwa hiyo wameona faida ya hifadhi, ila hapo kabla walikuwa hawajaelewa," alisema Dkt. Chande. "Wameona umuhimu wa kutunza hizi rasilimali. Hakuna mwananchi wa Mafia ndani ya hifadhi ambaye sasa anapenda kusikia bomu."
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dkt. Chande, kuna aina ya uvuvi wa kutumia nyavu za mitando ambazo haziruhusiwi kutokana na kuwa na macho madogo. Uvuvi huu bado unatumika katika vijiji viwili kwenye hifadhi ya Mafia. Lakini, alisema kitengo chake kinafanya jitihada za kudhibiti uvuvi huo. Hifadhi ya pili ni ya Mnazi Bay ambayo imeanzishwa mwaka 2000. Hifadhi hii inahusisha eneo lenye gesi la Mnazi Bay na ina ukubwa wa kilomita za mraba 650. Hapa uvuvi haramu ni mkubwa kutokana na kuwepo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika mkoa wa Mtwara.
"Doria imekuwa ngumu kutokana na kuwa wavuvi haramu wanapofukuzwa upande mmoja wa nchi wanakimbilia upande mwingine," alisema Dkt. Chande, akiongeza kuwa hata hivyo hali imeweza kudhibitiwa baada ya kuongeza nguvu ya doria katika hifadhi hiyo.
"Kwa sasa hali imekuwa nzuri, ilibidi usimamiaji wa sheria uwe mkali zaidi ili kupunguza upigaji wa baruti na wavuvi haramu wamepungua kwa kiasi kikubwa," kwa mujibu wa Dkt. Chande.
Alisema, “Hata hivyo, bado kuna vijiji viwili ambavyo vinasumbua katika kuendesha uvuvi haramu kwenye hifadhi hiyo.Lakini wamekuja wenyewe na kujisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya na kula kiapo mbele ya mwanasheria mkuu wa Serikali wakiahidi kuwa hawatarudia tena vitendo vyao vya uvuvi haramu, pia tumewaanzishia vikundi vyao vya doria ili wao wenyewe washiriki katika kusimamia hifadhi."
Akifafanua zaidi juu ya hifadhi hiyo, Dkt. Chande alisema ina rasilimali nyingi na vivutio viko vingi ikiwa ni pamoja na msitu mkubwa wa mikoko ambao usingekuwa katika maji hata wanyama wakubwa wangeweza kuishi humo. Pia kuna maingilio ya Mto Ruvuma ambayo yana viboko wengi na kuanzia mwezi wa nane kuna mapitio ya nyangumi. Watu wanavutiwa kuangalia nyangumi wakipita. Na ili kukuza utalii wa kuangalia nyangumi, ofisi ya hifadhi sasa imejengwa katika mapitio ya nyangumi. Ni kivutio kikubwa.
Pia kuna viota vya kasa ambavyo vinavutia watalii wengi wakati wa kuanguliwa kwa kasa na kuna vivutio vya matumbawe.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dkt. Chande utalii wa eneo hilo unakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa miundombinu.
"Vivutio viko vingi, lakini utalii bado haujakua kutokana na kukosekana kwa miundombinu. Barabara yetu ya Kibiti hadi Lindi haijaisha, hata usafiri wa kutoka (Mtwara) mjini kwenda eneo tulilojenga ofisi kilomita 45 ni barabara mbaya ambayo inahitaji uwekezaji," alielezea Dkt. Chande.
Hata hivyo, kuna watalii ambao wanapita vikwazo hivyo vyote kutokana na kupenda kufikia vivutio adimu vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Hifadhi ya tatu ni ile ya Tanga Coelacanth ambayo ilianzishwa mwaka 2009 ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 552. Ilianzishwa kwa shinikizo la Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na umuhimu wake wa kuwepo kwa samaki adimu duniani aina ya silikanti (Coelacanth). Pia ni kutokana na wananchi wenyewe wa Tanga ambao tayari wamehamasika kutunza mazingira na hivyo kuwasukuma kufika kwenye kitengo kuomba kuanzishwa kwa hifadhi.
Mbali na samaki aina ya silikanti, vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi ya Tanga ni pamoja na matumbawe, kasa na ni eneo lenye samaki wengi.
"Kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa hivi wananchi wenyewe wameanza kushuhudia kuwa samaki wameongezeka kwa kiasi kikubwa," alisema Dkt. Chande.
Maeneo tengefu
Kuna maeneo tengefu 15 nchini Tanzania huku Dar es Salaam pekee ikiwa na maeneo tengefu 7 ambayo yanapatikana upande wa Kaskazini na Kusini. Kwa upande wa Kaskazini kuna kisiwa cha Bongoyo, Mbudya na eneo tengefu la fungu la mchanga lijulikanalo kama Fungu Yasin na Pangamin.
Maeneo haya tengefu yalianzishwa kabla ya kitengo hakijaanza mwaka 1975 wakati Idara ya Uvuvi ilipokuwa inaanza. Maeneo hayo yalipitishwa kwa kutumia sheria ya Idara ya Uvuvi. Visiwa vya Kusini ni pamoja na kisiwa cha Finda, Kenda na Makatobe ambavyo vimeanzishwa na Kitengo cha Hifadhi za Bahari.
Ukiacha Hifadhi ya Bahari, Mafia pia ina maeneo tengefu katika visiwa vya Shungimbili, Nyororo na Mbarakuni.
Kwa upande wa Tanga, kuna kisiwa cha Maziwe katika Wilaya ya Pangani. Hiki kilipitishwa mwaka 1975 kuwa eneo tengefu ambapo wakati huo kilikuwa ni kisiwa. Lakini sasa kutokana na uharibifu wa mazingira, kimegeuka na kuwa fungu la mchanga. Kisiwa hiki kina mazalia makubwa ya kasa ambapo kuna utalii mkubwa unaoendelea wa kushuhudia jinsi kasa wanavyoanguliwa katika fukwe za Ushongo na Kikokwe.
Maeneo mengine tengefu yanaanzia Tanga mjini kwenda mpakani mwa Kenya. Maeneo hayo ni pamoja na Mwewe, Kilui, Ulenge na Kwale. Kisiwa cha Kilui kiko mpakani kabisa mwa Kenya. Hali hii imesababisha kitengo kuona haja ya kuanzisha usimamiaji wa pamoja wa maeneo tengefu na nchi za jirani. Hii itasaidia kudhibiti uvuvi haramu na kuhifadhi viumbe wanaohama kama vile kasa.
Tofauti ya Hifadhi za Bahari na Hifadhi za Taifa
Kuna tofauti kati ya Hifadhi za Bahari na Hifadhi za Taifa zilizopo chini ya Mamlaka ya Kusimamia Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Wakati hifadhi zinazosimamiwa na TANAPA haziruhusu wanajamii kuishi katika hifadhi za taifa, kitengo cha kusimamia hifadhi za bahari kinaruhusu wanajamii kuishi ndani ya hifadhi.
Kwa mujibu wa Dkt. Chande, mpangilio huu unafanya kazi ya kuwashirikisha wanajamii katika uhifadhi kuwa rahisi zaidi.
Mafanikio ya hifadhi na maeneo tengefu ya bahari
Moja ya mafanikio ni kuongezeka kwa akiba ya samaki baharini na kuhifadhiwa kwa rasilimali na viumbe bahari walio katika hatari ya kutoweka kama vile mikoko, matumbawe, kasa, nguva, silikanti n.k.
“Pia kuna ongezeko la utalii katika maeneo ya hifadhi, tunajaribu kuhamasisha utalii," alisema Dkt. Chande.
Eneo la bahari, ambalo kimsingi linaaminika lingetowa mchango mkubwa katika uimarishaji wa uchumi wa Taifa, limebaki na matumizi duni, hususan yale ya uvuvi wa kiwango cha chini yanayohusisha uvuvi wa vyombo, vifaa na teknolojia dhaifu, hivyo kushindwa kuleta tija yenye kukidhi haja.
Aidha, mbali na kuwepo mpango wa uanzishaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari kubwa ya kisasa katika eneo la Mpigaduri, kwa kipindi kirefu Zanzibar imebaki na bandari ndogo isiyoendana na wakati uliopo.
Kwa hakika hali hiyo inasabisha bandari hiyo kushindwa kukidhi mahitaji yaliyopo sambamba na kuhimili ushindani na bandari nyingine za Ukanda wa Afrika Mashariki.
Kuwepo kwa bandari za Mombasa na Dar es Salaam zinazohodhi eneo kubwa pamoja na vifaa mbalimbali vya kisasa, kumezifanya kuwa njia kuu ya kibiashara kati yake na mataifa ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika.
Lakini ‘penye ni pana njia’, juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. Ali Mohamed Shein ni biashara njema inayoonyesha muelekeo wa kuimarika kwa uchumi wa Zanzibar baada ya ujenzi wa Bandari hiyo kukamilika.
Pamoja na shughuli za kibiashara za uingizaji na utoaji wa bidhaa kutoka mataifa mbalimbali duniani, Zanzibar bado inabaki kuwa na fursa pana ya mafanikio katika matumizi ya bandari hiyo.
Shirika Ia International Maritime Organization (IMO) limebainisha kuwa asilimia 90 ya mizigo mizito duniani, husafirishwa kwa kutumia usafiri wa baharini, yaani njia ya meli.
Hivyo ni dhahiri kuwa bandari hiyo itakuwa kimbilio la makampuni na mataifa mbalimbali duniani katika usafirishaji wa mizigo yake.
Fursa nyingine inayoonekana kuimurikia Zanzibar, ni ile ya vijana wake kupata nafasi za ajira katika meli mbalimbali zitakazokuwa zikitumia bandari hiyo.
Kwa mantiki hiyo juhudi za makusudi zinahitajika kuchukuliwa na Serikali za kuharakisha ujenzi wa bandari ya Mpigaduri, sambamba na kufanikisha azma ya ujenzi wa Chuo cha Mabaharia hapa Zanzibar.
"Pamoja na kuwa lengo letu la msingi ni kuhifadhi mazingira, lakini baada ya kuhifadhi, mahitaji ya uwekezaji katika utalii yanazidi kuongezeka."
Changamoto za kuendeleza Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu
Changamoto kubwa ya kusimamia Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ni ulipuaji wa mabomu kutokana na kuongezeka kwa samaki katika maeneo hayo.
"Tunapata shida sana na uvuvi haramu katika maeneo hayo, baada ya kuyatunza samaki wamekuwa wengi wengi sana, kwa hiyo wahalifu wakilipua bomu na samaki kuelea wanachota samaki wengi. Kazi kubwa ni kusukuma utekelezaji wa sheria kwa kufanya doria za mara kwa mara ambazo ni za gharama kubwa. Hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uvuvi haramu," alisema Dkt. Chande.
Jinsi Serikali zinavyoimalisha uchumi wa bahari
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuimarisha sekta ya bahari ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dkt. Makame Ali Ussi akizungumza katika mafunzo ya siku tatu kwa wafugaji wa samaki na watendaji wa sekta za mazao ya bahari juu ya ufugaji wa mazao ya baharini katika ukumbi wa kituo cha kuzalishia vifaranga vya mazao ya bahari Bet al ras Bububu Wilaya ya Magharib A Unguja alisema Serikali inatambua umuhimu wa rasilimali za bahari ambazo zinachangia kutengeza mapato ya nchi pamoja na kuwawezesha wananchi kujikwamua na umaskini.
Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea na jitihada mbalimbali katika kutatua matatizo yanayowakabili wavuvi na wafugaji wa mazao ya bahari ikiwemo Majongoo, Samaki na Kaa.
Dkt.Makame alisema wakati umefika kwa sekta ya bahari kuendelea kuwa mhimili mkuu utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa chakula.
Alisema takwimu za uzalishaji wa mazao ya baharini zinaonyesha kuwa takribani asilimia 40 inawawezesha wananchi kunufaika na ajira ambapo asilimia 70 ya wananchi wanategemea sekta hiyo katika kujikwamua na umaskini jambo linalochangia ukuaji wa maendeleo nchini.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mifugo na Uvuvi, Dkt.Islam Seif alisema ili kuhakikisha wavuvi na wafugaji wanafikia malengo waliyoyakusudia Wizara itaendelea kushirikiana na wataalamu katika kutatua matatizo yanayojitokeza katika sekta hiyo.
Alisema mpaka sasa muitikio kwa wafugaji umekuwa mkubwa ambapo hadi kufikia wavuvi 49 elfu kutoka 35 elfu jambo ambalo linachangia maendeleo ya uchumi nchini.
Alitowa wito kwa wavuvi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wa maendeleo katika kuleta maendeleo pamoja na kuwa na matumizi mazuri rasilimali za bahari ili ziweze kuwanufaisha wananchi.
Mratibu wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya Samaki Bet al ras, Buriani Mussa alisema ni vyema kwa wananchi hususan vijana kuchangamkia fursa zilizopo za kujikita na ufugaji wa mazao ya baharini ili waweze kujingizia kipato cha uhakika.
Alisema si vyema kwa vijana kushindwa kushiriki katika miradi inayoanzishwa badala yake watafute njia mbadala za kuweza kujiajiri na kuachana na mawazo ya kusubiri ajira kutoka serikalini.
Washiriki wa mafunzo hayo, Naima Ibrahim na Semen Muhammed wenyewe waliomba kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kuzalisha mazao ya bahari yanayoendana na mahitaji ndani na nje ya nchi.
Walisema mbali na mafunzo pia ni vyema kwa wasimamizi wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya mazao ya bahari kufanya kazi kwa uhakika ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia ikiwemo kuondoa tatizo la upatikanaji wa vifaranga kwa wafugaji.
Mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu kwa lengo la kuwafunza wafugaji na wasimamizi wa mazao ya baharini namna bora ya kuimarisha ufugaji wa mazao hayo yaliwakutanisha pamoja wafugaji, wataalamu wa masuala ya bahari na watendaji wa Wizara ya Kilimo chini ya ufadhili wa FAO na KOICA pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Taarifa sahihi za viwango vya samaki tulionao zinaweza kuchochea ujenzi wa viwanda |
Meli ya kisasa ya utafiti wa samaki na mazingira bahari ya Dkt. Fridtjof Nansen imekamilisha uchunguzi wake wa rasilimali na mazingira bahari katika maji ya Bahari ya Hindi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ni meli ya tatu kubeba jina hili katika miaka 40 ya ushirikiano wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na nchi ya Norway. Ikiwa na maabara saba tofauti zenye vifaa vya kisasa kabisa, meli hii ya Dkt. Fridtjof Nansen ni chombo pekee cha majini chenye kupeperusha bendera ya Umoja wa Mataifa.
Chombo hiki kinaendesha tafiti kwenye nchi mbalimbali lengo likiwa kukusanya taarifa kuhusu mtawanyiko na uwingi wa samaki, bionuwai, hali za mazingira, na shughuli nyingine nyingi kwa kutumia teknolojia na vifaa vya kisasa kabisa kusaidia nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kukusanya taarifa za kisayansi muhimu kwa ajili ya uvuvi endelevu na kujua namna mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri bahari zao.
Chini ya Mpango wa Programu ya EAF-Nansen inayofadhiliwa na Norway na kutekelezwa na FAO kwa kushirkiana na Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Bahari ya Norway (IMR) meli hii inaendesha utafiti wake wa rasilimali bahari na mazingira baharini katika Ukanda wa Kusini Mashariki mwa Afrika na Bahari ya Hindi. Chini ya Programu hii, nchi thelathini (30) za Kiafrika ikiwemo Tanzania zitapata msaada wa kitaalam na kisayansi wa namna ya udhibiti wa rasilimali zao za samaki na viumbe bahari wengine kutumia na kutekeleza mpango endelevu wa utunzaji wa mazingira.
Akizungumza katika hafla fupi ya kilele cha utafiti huo katika pwani ya Tanzania iliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam ndani ya meli ya Dkt. Fridtjof Nansen, Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Mhandisi John William Kijazi alisema utafiti huo umekuja kwa wakati muafaka kwani ilikuwa inaenda kuongeza kasi ya uanzishwaji wa viwanda hapa nchini hususan katika sekta ya uvuvi. Alikuwa anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika hafla hiyo.
“Hii ni hatua kubwa sana kwa Tanzania ambayo itafaidika na huduma za utafiti wa kisasa wa meli hii kupitia ushirikiano wa wadau hapa nikizungumzia FAO na Serikali ya Norway, kuweza kujua kwa uhakika aina na kiwango cha samaki na rasilimali bahari nyingine tulizonazo katika maji yetu,” alisema na kuongeza: “Taarifa kuhusu rasilimali bahari zetu zitakuwa muhimu sana katika kufanya maamuzi na kupata fursa za ndani na kimataifa za uwekezaji katika sekta ya uvuvi huku tukitilia maanani mambo muhimu ya utunzaji wa mazingira. Kwa kutumia taarifa sahihi tunaweza kuwavutia wawekezaji waje na kujenga viwanda vya kusindika samaki na vingine vinavyohusiana na sekta hii ya uvuvi na hivyo kuongeza kasi kwenye mpango wetu wa kujenga Tanzania ya viwanda.”
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.Luhaga Joelson Mpina alisema kuwa ni matumaini ya Serikali kwamba takwimu zitakazotokana na utafiti huo zitaisaidia Tanzania kujua kwa uhakika juu ya aina na kiwango cha samaki na rasilimali bahari nyingine katika eneo letu la Bahari ya Hindi.
“Hii itatuwezesha kupata wawekezaji katika eneo hili ambao watajenga viwanda vya kuchakata na kusindika mazao ya samaki ambapo mbali ya kutoa fursa za ajira kwa watu wetu hususan vijana katika mnyororo wa thamani, lakini pia utakuza mapato ya serikali,” alisema.
Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania, Fred Kafeero alisema kuwa ushirikiano na Serikali ya Norway katika kutekeleza Programu ya Nansen ni wa umuhimu wa kipekee kwa FAO.
“Mbali ya taarifa ambazo zitawezesha udhibiti bora wa rasilimali kwa matumizi endelevu, utafiti huu utapelekea uelewa mzuri wa athari za mabadiliko ya tabia nchi na athari nyingine za nje, kama vile uchafuzi wa mazingira na mifumo ya uhai baharini,” alisema.
Kwa upande wake, Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad, alisema: “Ni matumaini yetu kuwa meli ya Nansen itachangia siyo tu katika kuhakikisha kuwa takwimu za uhakiki za kisayansi zinapatikana, lakini pia kuimarisha uwezo katika matumizi ya takwimu hizo ili kujenga mikakati bora ya udhibiti na matumizi ya rasilimali bahari.
Bahari zina utajiri mkubwa kuanzia ufugaji wa samaki, uvuvi na pia uchakataji na usindikaji wa mazao ya samaki. Sera zenye kutilia maanani taarifa hizi ni muhimu katika kujenga msingi kwa ajili ya viwanda vipya kama vile uchimbaji wa madini katika sakafu ya bahari na kilimo pamoja na uvunaji wa mwani na viumbe vingine, na hivyo kuchangia katika juhudi za maendeleo kwa Tanzania.”
Hafla hii iliandaliwa kwa pamoja kati ya FAO kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway hapa nchini na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na ilihudhuriwa na Mawaziri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Mabalozi na wakuu wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa na Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Chimbuko
Programu ya Udhibiti na Matumizi Endelevu ya Rasilimali Samaki (EAF) – imekuwa ni moja ya marejeo makuu ya FAO katika kusaidia nchi katika juhudi zao za kudhibiti na kutekeleza kanuni za maendeleo endelevu.
Kanuni za FAO za Uvuvi Sahihi na pia sheria nyingi za kimataifa zinaangazia faida ambazo zinaweza kupatikana kupitia programu ya EAF. EAF ni njia ya kutekeleza Kanuni Sahihi za Uvuvi kwa kutoa muongozo wa namna ya kufikia malengo, sera ya kiuchumi, kijamii na ikolojia kupitia malengo, viashiria na njia za tathmini.
EAF inanuia kuweka uwiano kati ya mambo mawili muhimi: utunzaji wa mazingira na mifumo ya ikolojia kwa upande mmoja na kuweza kutatua mahitaji ya binadamu ya chakula na faida za kiuchumi upande mwingine.
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi na FAO wamesaini mkataba wa programu ya ushirikiano kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya EAF-Nansen huku Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Bahari ya Norway (IMR) ikitoa huduma ya kisayansi.
Programu mpya ya EAF-Nansen imeongeza eneo jipya la kushughulikia ambalo linaangalia athari za tofauti na mabadiliko ya tabia na uchafuzi wa mazingira yanavyoathiri uzalishaji wa mazingira bahari na afya.
Serikali: rasilimali za bahari zitumike kwa maslahi ya Watanzania
Serikali imesema kuwa itahakikisha rasilimali za bahari zinatumika kwa ajili ya Watanzania wote.
Hayo aliyasema Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid alipofanya ziara ya ukaguzi wa meli ya uvuvi katika bandari ya Zanzibar.
Rashid alisema kuwa rasilimali za baharini zikitumika ipasavyo zinaweza kuleta maendeleo na kuhakikisha uvuvi unaofanyika katika bahari unafuata taratibu kwa maslahi ya taifa.
Katika ukaguzi huo wa meli hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Abdallah Ulega walitembelea ofisi za utoaji leseni wa meli za uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alisema sheria iko wazi kwa hivyo lazima rasilimali za Tanzania ikiwemo na bahari iwanufaishe Watanzania wote bila kujali vyama vyao.
Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema Serikali zote mbili zitahakikisha rasilimali za bahari zinatumiwa na Watanzania na siyo kwa wageni tu.
Alisema watasimamia sheria za uvuvi katika kulinda rasilimali za bahari ili ziweze kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Hosea Mbilinyi alisema mamlaka imepiga hatua katika kuhakisha rasilimali za bahari zinanufaisha Tanzania.
Mazingira Endelevu kwa rasilimali bahari
Mazingira ni nini? Mazingira ni vitu vyote vyenye uhai na visivyoishi ambavyo vinatuzunguka vitu vya maumbile na vilivyofanywa na binadamu.
Mazingira yanajumuisha vitu vyote visivyoishi kama vile hewa tunayovuta maji tunayokunywa, barabara na nyumba, bahari na fukwe, hata jua, mwezi na vyota. Mazingira pia ni pamoja na vitu vyenye uhai kama mimea: misitu na mashamba makubwa, mibuyu, vichaka na nyasi, mikoko, mwani, nyasi bahari, miamba ya matumbawe na mazao, na wanyama wakiwemo wanyama pori, samaki, vipepeo, ndege, nyuki, wanyama wanaofugwa na watu.
Kila kitu kilichopo karibu yako ambacho unaweza kukiona, kukigusa, kukihisi, kukinusa au kukisikia ni sehemu ya mazingira. Mazingira yanatupatia nini? Chakula na maji. Katika Zanzibar maji yetu safi yote yanapatikana kutoka maji ya mvua ambayo huzama ndani ya ardhi. Hujichuja kupitia mawe ya chokaa, nasi huchimba visima ili tupate maji ya kunywa, kupikia na kuoshea.
Samaki wote tunaokula ni viumbe wanaokamatwa baharini, na mifugo yetu pia inategemea chakula na maji ya kunywa, mazao kama mpunga, matunda na mbogamboga yanahitaji udongo mzuri wenye rutuba, mvua nyingi na nyuki, ndege na popo ili kurutubisha.
Bila ya mazingira wangelikula na kunywa nini? Afya njema – Mimea hupunguza kasi ya umwagikaji wa maji yanayotiririka juu ya ardhi kwa hiyo yanazama ardhini ambako yanachujwa na mawe, na hiyo hufanya maji yawe salama zaidi kunywa.
Hewa safi (oxijini) iliyomo kwenye hewa tunayovuta ambayo inatupa uhai inatolewa na mimea nayo huchukua na kutumia hewa chafu kutoka kwenye hewa. Pia, sisi tunatumia mimea mingi inayoota Zanzibar katika kutibu magonjwa, kuanzia malaria hadi mafua: inasaidia kutuweka katika afya njema.
Mahali pa kuishi
Ukiangalia baharini kwenye ufukwe wa mashariki ya Zanzibar unaweza kuona wapi mwamba ulipo, kwa sababu ya mawimbi makubwa yanayoonekana wakati yanagonga mwamba huo. Lakini ikiwa mwamba huu hautakuwepo na kupiga kwenye ufukwe inaweza kusababisha mmomonyoko.
Miamba ya matumbawe, nyasi bahari na mikoko yote hulinda ufukwe dhidi ya mmomonyoko. Ardhini, miti na nyasi (majani) inafanya hivyo hivyo, inazuia udongo usiondolewe na kupelekwa baharini inaponyesha mvua. Bila ya vitu hivyo ardhi iliyopo chini ya nyumba zetu ingeondolewa na nyumba zetu zingeharibiwa hata kupelekwa baharini. Miti hutupatia kivuli na kuzilinda nyumba zetu dhidi ya upepo mkali. Nyumba zetu zimeezekwa kwa makuti ya minazi, mawe mchanga, saruji na miti ya mikoko: vifaa hivi vyote vinatokana na mazingira.
Maisha na ustawi wa kiuchumi
Kazi nyingi katika Zanzibar zinategemea mazingira. Asilimia 39 ya watu wameajiriwa katika sekta ya huduma (sana kwenye utalii), na asilimia 37 katika kilimo, Misitu na Uvuvi. Uchumi wote wa Zanzibar unategemea mazingira mazuri.
Maliasili Mazingira yanatupatia kila kitu tunachotaka kwa maisha. Vitu tunavyotumia tunaviita ‘rasilimali’. Rasilimali zinaweza kuwa vitu halisi, kama hewa safi au maji au rasilimali za nishati kama mwangaza wa jua au upepo.
Vitu vyote vinavyofanywa na binadamu vinafanywa kwa kutumia rasilimali ambazo hatimaye vinatokana na mazingira ya kimaumbile yanayojulikana kama ‘mali asili’. Kwa mfano saruji inafanywa kwa kuchoma chokaa, plastiki hufanywa kutokana na mafuta, na vioo vinafanywa kutokana na mchanga. Lakini mali asili zinatoka wapi? Mara nyingi, watu hufanya mambo kama vile rasilimali zote zitadumu milele, lakini kama idadi ya watu inavyoongezeka, baadhi ya rasilimali zinaadimika sana. Kwa hivyo tunapaswa tufikiri tunapotumia vitu: vimefanywa kutokana na nini? Vitu asili vimetoka wapi? Kiasi gani cha vitu hivyo watu wanatumia? Inaweza kumalizika?
Uendelevu
Nini maana ya kuwa endelevu? Kuwa endelevu maana yake ni uwezo wa kuendelea kuwepo. Tunategemea mali asili, kwa hiyo tunazihitaji ziwepo (siku za usoni) kwa ajili ya watoto wetu. Katika muktadha wa maliasili kuweza kuwa endelevu maana yake ni kutumia rasilimali siyo kwa haraka kuliko inavyoweza kupatikana tena. Tunahitaji kutumia rasilimali kwa uangalifu sasa, au hazitakuwepo tena baadae.
Rasilimali zenye kurudishwa upya na zisizoweza kurudishwa upya, Aina mbali mbali za rasilimali hufanywa kwa mchakato wa kimaumbile katika kasi ya mwendo tofauti na kwa viwango tofauti. Kwa mfano, mwanga wa jua hufanywa mchana wa kutwa, kila siku, lakini mibuyu mikubwa huchukua mamia ya miaka mpaka ikawa mikubwa kiasi hicho.
Tunapotumia rasilimali, tunahitaji kuzingatia muda ambao rasilimali hizo zitachukua kujirudi kuwa kama hali ya mwanzo. Iwapo tutatumia kwa haraka rasilimali kuliko ambavyo zinaweza kurejea, basi zinaweza kumalizika. Huku siyo kuwa endelevu. Ili kuhakikisha tunazo rasilimali hizo tunazohitaji siku za usoni, ni lazima sote tuishi kwa kuzitumia kwa njia endelevu, tusitumie rasilimali kwa haraka kuliko zinavyoweza kurejeshwa.
Tunazingatia kiwango cha kurejesha rasilimali katika muda wa maisha ya mwanadamu. Iwapo maumbile yanarejesha vitu katika muda wa maisha ya mwanadamu tunaviita vitu hivyo vinarejesheka.
Maana yake ni kuwa maumbile yanaweza kuweka tena rasilimali tunazotumia. Rasilimali hizi ni pamoja na maji safi, ambayo yanarejeshwa na mvua inaponyesha, kuni, zinarejeshwa miti mipya inapoota, samaki wanarejeshwa na samaki wapya wachanga, na nishati ya jua au upepo. Lakini vitu ambavyo huchukua muda mrefu zaidi kuliko uhai wa mwanadamu huitwa visivyorejesheka.
Rasilimali zinaporejesheka
Baadhi ya rasilimali hazina kikomo – hutengenezwa kwa wingi kiasi ambacho zipo zaidi ya tunazotumia, kwa mfano hata tukitumia kiasi gani cha nishati ya mwangaza wa jua au upepo leo (kwa mfano kwa kuchemsha maji kwenye jua au kuendeshea jahazi au mashua) hazitozima jua kung’ara (kutoka mwangaza) au upepo usivume kesho.
Hii ina maana tunaweza kutumia kiasi tunachopenda cha rasilimali hizi, na bado zitakuwa zinaendelea na kupatikana! Rasilimali nyingine huchukua muda mrefu zaidi kurejeshwa kimaumbile (wenyewe), zinachukua miezi, miaka, au hata miongo kabla hazijarejeshwa kimaumbile. Kundi hili ni pamoja na rasilimali hai nyingi kama samaki na kuni na maji safi, ambayo yanarejeshwa katika msimu wa mvua.
Tunapokata miti kuitumia kwa kuni au mbao lazima tupande mingine mipya. Tunapokwenda kuvua samaki, lazima tuwabakishe wengine ili wazae samaki wengine. Lakini iwapo tutakata miti yote na kuwauwa samaki wote au kuyavuta maji yote kutoka ardhini, hakutakuwa na kilichobaki kwa siku za usoni.
Rasilimali zisizorejesheka, Rasilimali nyingine tunazotumia zilichukua maelfu au mamilioni ya miaka kufanyika, mara nyingi katika hali ya mazingira tofauti na hizi ya sasa. Kwa hiyo kwa mtazamo wa kibinadamu rasilimali hizi hazirejesheki.Tukishatumia kile kilichopo sasa hakitakuwapo tena.
Rasilimali zisizorejesheka ni pamoja na kisukuku cha fueli, makaa ya mawe, mafuta, gesi, na vitu vinavyotengenezwa kutokana navyo, pamoja na plastiki. Nyingine ni rasilimali za madini mawe na mawe ya thamani. Uchimbaji wa rasilimali hizi na gharama nyingine za kimazingira tunahitaji kutafuta rasilimali mbadala, zenye kusarifika na kuendelea ili tusizitumie sana.
Kwa nini kuwa endelevu ni muhimu?
Tunategemea mazingira kwa namna nyingi mno kwa ajili ya kujipatia riziki, lakini iwapo haturuhusu rasilimali kuongezeka kutokana na kutumiwa sana, basi samaki tunaokula watatoweka, hatutakuwa na kuni za kupikia, wala maji ya kunywa.
Kama vile tunavyotegemea mazingira nayo yanatutegemea pia kwa sisi kuyaangalia na kuyatumia kwa busara. Lakini hatutumii rasilimali kiuendelevu. Misitu katika Zanzibar inapungua kwa kasi, idadi ya samaki inapungua. Kiwango cha maji yaliyopo ardhini kinashuka na visima vya pwani vinakuwa na maji chumvi na yasiyonyweka.
Rasilimali zinaondoka, na iwapo hatutachukua hatua sote kuanzia sasa tutakuwa katika shida kubwa baadae. Huu ndiyo mustakbali ambao vijana wa Zanzibar wataurithi. Kwa hivyo tunaweza kufanya nini? Tuko katika kipindi cha historia ambacho bado zipo rasilimali, tunaelewa athari tunayopata, na bado tunao muda wa kuchukua hatua.
Ni juu yetu kubadili namna tunavyotumia rasilimali na tuzitumie ili zidumu, kuanzia sasa. Ni vizuri kuvua samaki lakini siyo wengi kiasi ambacho hawabaki kwa siku za usoni. Samaki wanahitaji muda kukua, kupata mwenza wa kuzaa kama watu na wanyama wa kufugwa wanavyofanya. Miti pia inahitaji muda kukua – tusikate miti kwa haraka sana kuliko inavyoweza kuota na kurejea.
Bioanuwai
Bioanuwai ni nini? Bio maana yake ni maisha, na anuwai ni aina, kwa hiyo, bioanuwai ina maana ya aina ya maisha. Inajumuisha vitu vyote vinavyoishi duniani na katika bahari, kuanzia nyangumi wakubwa kabisa mpaka bakteria wadogo kabisa.
Mahali ambapo aina nyingi tofauti, au ‘spishi’, au vitu vyenye uhai hukua pamoja, kama vile mwamba wa matumbawe au msitu, panasemekana kuwa na bioanuwai nyingi, na mahali ambapo pana spishi chache, kama shamba lililolimwa, au maeneo ya mjini, pana bioanuwai wachache.
Spishi adimu, kuwa na spishi nyingi sio jambo la pekee muhimu lakini ni muhimu pia (kujua) kama spishi hizo zinapatikana mahali pote. Spishi adimu ni maalum sana. Kwenye visiwa, kwa sababu makundi ya mimea na wanyama wametengwa na bahari na makundi mengine ya mimea na wanyama, pole pole wanabadilika kuweza kujirekebisha kwa hali za hapo.
Baada ya muda, mimea na wanyama hao huwa tofauti sana na jamaa zao kiasi cha kuwa spishi mpya. Sehemu za visiwa kwa hivyo, ni muhimu sana kwa viumbe anuawai kwa sababu kunaelekea kuwa na spishi adimu zaidi kuliko maeneo ya bara yenye ukubwa kama huo.
Bioanuwai katika Zanzibar: makazi na spishi Makazi ya baharini, Kuna aina nyingi tofauti za makazi ya baharini katika Zanzibar kuanzia ufukweni mpaka kwenye bahari iliyo wazi. Kila makazi yanamudu mamia ya spishi, na bioanuwai katika Zanzibar ni maarufu duniani kote.
Spishi nyingi huishi sehemu ya maisha yao katika makazi moja na waliobaki huishi mahali pengine, kwa hiyo makazi ya bioanuwai ni muhimu sana.
Makazi ya chini ya maji ni vigumu kuyagundua, lakini kuna mengi ya kugundua kwa kutembea tu ufukweni na sehemu za baharini wakati wa maji kupwa.
Kwa mara ya kwanza, fukwe zenye mchanga zimeweza kuonekana hazina viumbe isipokuwa minazi.
Lakini viumbe wamejificha hapa – lazima ujue pa kutazama. Chimba chini kidogo tu na unaweza kuona chaza; kaa pepo wanaishi katika mashimo na hutembea kwa haraka sana, kwenye fukwe na unaweza kuwaona kwa shida; kaa watawa wamejificha vile vile katika makome ya viumbe wengine.
Fukwe zenye mchanga ni muhimu kwa makazi ya matagio ya kasa, ambao huja ufukweni usiku na kutaga mayai yao chini ya mchanga. Zanzibar inao spishi za kasa bahari, maarufu wao ni kasa wa kijani (green turtle) na kasa wa kawaida (hawksbill).
Fukwe zenye mchanga hutumika pia kwa ndege malapulapu ambao wanakula samaki na kombe: korongo, bua bua, ndoero, na wengine wengi. Fukwe za maweni ni mahali muhimu kwa kuangalia bioanuwai wa baharini.
Vidimbwi vyenye mawe vinaweka anemone, kaa, mwanamizi na samaki wachanga, na wanyama kama kombe wa baharini. Aina ya konokono bahari (littorina) na ‘barnacles’ ambao wanaambatana na miamba na kuganda chini ya vyombo. Sehemu hizi asilia za kujionea samaki na viumbe wengine ‘aquarium’ vinakufanya uone aina nyingi tofauti za viumbe wa kushangaza bila ya kuwasumbua. Ukibahatika sana unaweza kuona hata pweza. Wanyama wengi unaoweza kuwaona ni wa ajabu kuliko unavyoweza kufikiria!
Maji yanapokupwa mfumo mwingine wa ekolojia unaonekana, vitalu vya nyasi bahari vinaota katika mchanga na matope. Nyasi bahari zinasaidia viumbe wengi wa kuvutia sana majongoo bahari, mwanamizi na aina nyingi za kombe / chaza. Kwenye vitalu vya nyasi vya maji mengi, kasa wanakula majani pia.
Kati ya mifumo yetu ya ekolojia ya baharini inavutia sana ni miamba ya matumbawe. Chini ya mawimbi yamejificha mamia ya spishi ya matumbawe yenye rangi za kung’ara, sponji, kaa, kamba wakubwa, samaki wa miamba, papa, taa na mara nyingine hata wanyama wakubwa duniani nyangumi (whale shark).
Mbali na miamba katika bahari kuna viumbe wa ajabu sio haba wanyama wa hapa petu tu ni spishi 8 za pomboo, 3 za nyangumi na aina moja ya nguva (dugong). Mfano wa aina za pomboo ni pomboo kikomo, pomboo madoto, pomboo mweusi pia nyangumi mwenye nundu, wote wanapatikana katika Ghuba ya Menai. Msitu pori – Miti huipa misitu muundo ambao hutoa sehemu nyingi kwa spishi kupata makazi.
Kila spishi za miti zinavyoota msituni ndivyo inavyosaidia bioanuwai wengi zaidi. Misitu ya pwani ya Afrika ya Mashariki inafanya mojawapo ya maeneo ya misitu 25 muhimu ya bioanuwai duniani. Kuna aina tatu kuu za misitu pori katika Zanzibar. Msitu mnyevunyevu hustawi na ni kijani sana.
Miti hukua haraka, mikubwa na mirefu, na majani yao yanapoanguka, huoza na kufanya udongo mnene wenye rutba. Sehemu kubwa ya msitu mnyevunyevu ya Zanzibar ipo Pemba, lakini upo msitu mnyevunyevu Unguja Kaskazini na Jozani.
Msitu unaoota pembezoni mwa fukwe kwenye mawe mawe huota katika maeneo yenye mvua kidogo, na miti yake inaweza kuhimili ukame. Huota katika Ukanda wa matumbawe chokaa ambayo inapitisha maji kwa urahisi, kwa hiyo maji ya mvua hupotea haraka.
Maeneo makubwa kabisa ya msitu wa aina hii inayokuwa juu ya mawe katika Zanzibar yapo Kusini Mashariki ya Unguja. Mikoko huota Ukanda wa pwani na inavumilia chumvi. Mikoko ni muhimu kwa sababu inazaa sana (miti yake huota haraka) na ukuaji huu hutoa chakula kingi kwa wanyama pori. Visiwa vyote viwili vikuu vinahimili mikoko mikubwa na muhimu ambayo inafanya kazi ya sehemu za malezi kwa samaki wengi wanaoishi baadae katika miamba ya matumbawe. Zanzibar ni nyumba ya zaidi ya spishi 50 za wanyama wakiwemo wanyama wa hali ya juu kama nyani, kima punju adimu kima bluu Sykes’ na spishi tatu za komba.
Tunazo spishi mbili za paa, akiwemo paa nunga (Ader’s duiker) ambaye yupo hatarini kutoweka: wamebaki chini ya 500 duniani karibu wote wakiwa Zanzibar. Pia tuna spishi 23 za popo pamoja na popowa wa Pemba anayeruka (flying fox).
Popo wadogo hula wadudu, na wakubwa hula matunda. Mojawapo ya kivutio kisichoaminika au kinachoshangaza cha Zanzibar ni uhamiaji wa popo wanaokula matunda wakati wa kutua jua wanapotoka visiwa vilivyoko baharini, ambako hulala mchana na kuelekea msituni ambako hula wakati wa usiku.
Zipo spishi 177 za ndege, pamoja na chozi ambaye ana rangi inayong’ara, tai adimu na chiriku ambao ni shida kuwaona lakini sauti zao nzuri ni rahisi kuzisikia, hususan kabla ya jua kuchomoza.
Pemba ni maarufu kwa ndege wake adimu: kinengenenge wa Pemba, njiwa manga wa kijani wa Pemba, chozi wa Pemba na bundi wa Pemba. Zipo spishi kadha za nyoka na mijusi, maarufu sana ni kinyonga, anayeweza kubadili rangi yake ioane na mazingira! Wapo baadhi ya wanyama wadogo wadogo maalum pia, wakiwemo kaa mnazi mkubwa adimu (coconut crab), na maelfu ya wadudu: vipepeo vizuri, kerengende wanaocheza, vimetameta na ‘mwindaji’ anayevamia kwa kushambulia, na vunja jungu.
Ardhi ya binadamu
Sehemu kubwa ya ardhi ya Zanzibar imebadilishwa na wanadamu kuwa ardhi ya kilimo, vijiji na miji. Lakini wapo bioanuwai hapa. Ardhi ya kilimo ni muhimu kwa ndege, nyuki, na vipepeo na kutoa nafasi ambayo wanyama pori, wanaweza kuitumia katika kwenda katika maeneo ya misitu ya kimaumbile.
Hata vijijini kuna wanyama pori, kwa vile spishi nyingi za msituni zinaweza kuishi miongoni mwa binadamu, mradi tunawachia miti na vichaka baina ya nyumba zetu.
Kwa nini bioanuwai ni muhimu?
Bioanuwai ni muhimu kwa sababu viumbe hai wanategemeana kwa chakula na mahali pa kuishi na kuzaa.
Viumbe hai kama sisi wenyewe ni sehemu ya mtandao wa maisha, na sisi pia tunategemea vitu mbalimbali vinavyoishi kwa chakula chetu, kwa hewa tunayovuta na kwa njia zetu za kujipatia riziki. Iwapo tutauvuruga uwiano wa maumbile kwa kusababisha spishi kufa, mfumo unakuwa siyo sawa na mfumo mzima wa ekolojia unaweza kuharibika. Mara nyingine hali hii huyafanya maeneo yasikalike kwa watu kwa mfano yanaweza kugeuzwa jangwa: iwapo miti yote itakatwa, udongo hupeperushwa na mimea kidogo tu inaweza kuota.
Mimea inatoa oxijini (hewa safi) tunayoihitaji ili tuishi. Mimea inayoota hufyonza gesi hatari, na kupunguza athari ya mabadiliko ya hali ya hewa. Dunia ya kimaumbile ni nzuri; watu wanaoishi au wanaotumia muda katika maeneo ya kimaumbile wana afya zaidi kuliko wale wanaoishi katika maeneo ambayo hewa imechafuliwa.
Maelfu ya mimea hutumika katika dawa za asili za Zanzibar. Ni muhimu kuhifadhi aina mbalimbali za viumbe wa msituni ili kuilinda mimea hii, na mingine pia, kwa vile wanasayansi wanatafuta tiba mpya na bora.
Maji – Misitu husababisha mvua kwa kupunguza mwendo wa mawingu yanapopita juu kwenye ardhi: miti na mimea huyachuja maji na kuyafanya maji ya chini ya ardhi salama kwetu kuyanywa.
Maeneo yaliyo na miti na mimea mingi hupunguza mwendo wa maji yaliyopo juu ya ardhi, kwa hiyo maji huzama ndani ya ardhi badala ya kutiririka na kuupeleka udongo baharini. Chakula bioanuwai hutupatia mamia ya samaki tunaokula na miti au mbao tunazohitaji kutengenezea mitego na kujenga mashua za kuvulia, na moto wa kupikia. Wadudu, popo na ndege wote wanasaidia kuchavusha mazao tunayolima.
Viumbe waliomo katika udongo vile vile ingawa ni wadogo sana, kiasi cha kutoweza kuonekana, huyavunja majani ya miti iliyokufa na kuyageuza yawe udongo wenye rutuba kwa kupanda mazao, ndege, nyoka na wadudu wanaokula wengine wanakula wadudu wanaoharibu mazao.
Malazi, miti hupunguza athari ya upepo katika dhoruba na hutoa kivuli kutokana na jua kwa ajili ya familia zetu, nyumba, mifugo na mazao.
Malighafi tunayotumia kujengea nyumba zetu – aina mbalimblai za mbao, miti, mapaa, na chokaa vyote vinatokana na vitu vya maumbile. Njia za kujipatia maisha (riziki) Utajiri wa wanyama pori wa Zanzibar unavutia maelfu ya watalii kila mwaka kutembelea msitu wa Jozani, kuogelea na pomboo, kuzamia ndani ya maji na kupiga mbizi chini ya maji.
Wafanyakazi wote katika kazi ya uvuvi, kilimo au utalii wanategemea aina nyingi za wanyama na mimea mikubwa na midogo kwa kupata riziki zao.
Kwa nini wanyamapori wa Zanzibar wamo hatarini?
Inapokuwa idadi ya spishi iko chini au inapungua, spishi hiyo imo katika hatari ya kutoweka kabisa, au ‘imo hatarini’.
Hii inaweza kuwa kwa sababu ya tishio kwa mmea au mnyama mwenyewe, au kwa sababu makazi yake mahali anapoishi panaharibiwa au panatoweka.
Binadamu wanashindana na mimea na wanyama katika Zanzibar kwa rasilimali na nafasi ya kuishi, na baadhi ya spishi tayari wameshapotea bioanuwai inapungua Zanzibar. Kuuliwa moja kwa moja Spishi nyengine zinauliwa makusudi.
Tunavua idadi kubwa ya samaki kila siku kwa ajili ya chakula, na watu wengine pia huwinda paa. Tunakata miti kwa ajili ya kuni, mkaa, mbao za kujengea nyumba, mashua na ngalawa, na samani. Spishi nyingine wanavuliwa kwa sababu ya kibiashara baragume ‘tritoni’, kombe, chaza na magamba ya kasa yanauzwa kama mapambo, na mapezi ya papa yanasafirishwa nje ya nchi.
Tunawauwa baadhi ya wanyama kama nyoka kwa sababu tunawaogopa. Mara nyingine kuwauwa moja kwa moja sio makusudi; pomboo na nyangumi wa baharini na kasa hukwama katika nyavu. Uuwaji wa moja kwa moja usio dhibitiwa una athari kubwa sana katika idadi yao na wengi wa spishi hizo wamo hatarini wakiwemo papa, kasa, pomboo, na baragumu. Kuna spishi moja, ambayo ilikuwa ya aina yake kwa Zanzibar lakini tumeshachelewa.
Chui wa Zanzibar aliwindwa mpaka akatoweka kabisa katika miaka ya 1990. Upoteaji wa makazi kutokana na udhalishaji na uharibifu Tunaharibu miamba ya matumbawe baharini na vitalu vya nyasi bahari kwa kutumia vifaa vya uvuvi kama nyavu ya kukokota na baruti.
Maendeleo ya pwani na mmomonyoko wa ardhi inasababisha kasa wasiweze tena kupata mchanga mkavu ufukweni kwa ajili ya kutaga mayai yao na kulalia wakati wa usiku. Kasa wachanga huchanganyikiwa kutokana na mwanga mkali unaotoka hotelini, kwa hiyo, hupotea na hawawezi kuijua njia ya kwenda baharini!
Uchimbaji wa mchanga na mawe ya chokaa ni tatizo kubwa sana katika fukwe na hata ndani kwenye ardhi. Misitu inakatwa Zanzibar, lakini hususan katika ukanda wa pwani ili kupisha kilimo, barabara, nyumba na hoteli: kilimo cha kuhama hama kukata au kuchoma eneo la msitu kwa ajili ya kupanda mazao, halafu kwenda katika eneo jingine baada ya miaka michache bado inaendelea, lakini namna kinavyofanywa sasa siyo endelevu.
Kimila mashamba ya zamani yaliachwa ili misitu iote tena, lakini sasa watu wengi sana wanahitaji ardhi ya kulima kiasi cha kuwa msitu hauachwi uote tena. Spishi haribifu Mara nyingine, watu wanapokwenda duniani huchukua wanyama na mimea kutoka mahali pamoja na kuwaanzisha mahali pengine, ambapo si pao.
Kwa kawaida hawaishi, lakini iwapo hawana wanyama wanaokula wenzao katika hapo mahali papya, wanaweza kuzaa kwa haraka sana na kuangamiza idadi kubwa ya mimea au wanyama wa hapo, na kuchafua usawa wa kimaumbile wa mfumo wa ekolojia.
Meli hupeleka panya visiwani ambapo kwa haraka sana huwamaliza ndege wanaojenga ardhini. Spishi haribifu mbaya kabisa wa Zanzibar ni kunguru wa nyumbani aliyeingizwa kutoka India.
Kunguru wapo kila mahali, wanakula uchafu wa chakula na mboga na ndege wa kienyeji na mayai yao, mijusi, vyura na wanyama wengine wadogo. Idadi ya spishi za kienyeji zinapungua Zanzibar pote, lakini hasa Pemba ambako wawili kati ya spishi nne za ndege adimu wanahofiwa wametoweka sasa.
Paka wa kufugwa wanaweza kusababisha matatizo iwapo wataingia porini, wanazaa kwa haraka, hawana wanyama wanaowala, na wanakula vinyama vidogo, ndege na mijusi. Uchafuzi wa hewa Usimamiaji wa takataka katika Zanzibar hautoshelezi, na plastiki, kemikali, maji machafu na vitu vingine vingi vinasababisha matatizo makubwa kwa bioanuwai.
Kemikali hususan dawa za kuulia wadudu, sumu ya wanyama pori, vipande vya plastiki vinapenya kuingia kwenye mazingira ambako wanyama wengi wanaufananisha na chakula, kwa hiyo matumbo yao hujaa na kwa hiyo hufa kwa njaa.
Uchafuzi wa hewa unachangia katika ongezeko la idadi ya kunguru wa majumbani kwa njia isiyo dhahiri, kwa kusababisha athari ya kupungua kwa wanyama pori. Ilikuwa tayari ni nadra ulipochapishwa huu mhuhuri mnamo 1984, Chui wa Zanzibar tayari ameshatoweka.