Ofisi Ambayo sio Halisi — Lakini upo nayo muda wote

Watu wengi walikuwa wakielewa maana ya ofisi kama Mahali pa kazi palipo na mlango maalum, huduma nzuri kama maji baridi, na saa inayokuaminisha sasa ni wakati umemaliza kazi za siku. Lakini hali hii imeanza kutoweka. Sasa, ukitumia kompyuta yako mahali popote hata juu ya meza ya jikoni ni ofisi kamili sawa kabisa na jengo lolote la vioo. Hakuna tena kuingia ofisini na kusalimiana na watu wengi ndani ya lifti, unaingia mtandaoni tu na kuanza kazi.
Hali hii inafanana na gemu. Mwanzoni, una uhuru hakuna malengo ya haraka, hakuna shinikizo. Ni nafasi tupu, Lakini taratibu, gemu huanza kuonyesha mpangilio wake. Bado una malengo, Bado kuna mipaka, hata kama haionekani mwanzo.
Majukwaa mengine yanayoelezea mabadiliko haya katika michezo ya gemu na pia katika utamaduni wa kazi yameanza kufuatilia mienendo hii. Unaweza kubofya hapa kwa mifano ya jinsi Gemu (Michezo) bila sheria bado inaweza kuathiri tabia, na jinsi kufanyia kazi nje ya ofisi inafuata mantiki hiyo hiyo ya ajabu.
Pale Kulipokuwa na Kuta za Ofisi, Sasa Kuna Muda Tu
Watu walidhani kutokwenda ofisini kutawaweka huru na huenda ilifanya hivyo. Hakuna safari za kwenda kazini, hakuna mikutano mingi. Lakini muda wa kazi umeongezeka. Watu wengi wamejikuta wakifanya kazi masaa mengi Zaidi kuanzia asubuhi, machana mpaka usiku bila kuzingatia muda maalum wa kazi wakijikuta kila nafasi aipatayo yupo kwenye komputa yake na kupumzika kwa udogo sana.
Na si kwamba kuna mtu anakulazimisha, Ndicho kinachoshangaza Zaidi, Uko huru lakini kwa namna fulani upo kazini kila wakati. Hakuna kengele, Hakuna tuonane kesho. Unafunga tu kompyuta yako, na dakika tano baadaye yanakujia mawazo ya uwashe aungalie kama kuna email yoyote au kama faili limepakiwa vizuri.
Wapo Wanaopenda Hali Hii
Kwa baadhi ya watu, maisha haya ni sawa. Wanatembea na mbwa saa tano asubuhi, Wapika chakula cha mchana, Wanajibu barua pepe wakiwa katika mazingira yao ya kufurahia maisha maeneo mbalimbali. Kwao, kazi nisehemu ya maisha yao ya kila siku na sio maisha yao ni sehemu kazi. Hawahitaji ratiba wanahitaji malengo tu.
Na huenda hawakupenda mfumo wa zamani pia. Hawaukumbuki uwanja wa maegesho ya magari kazini, mavazi ya kikazi, au kukaa kazini hadi saa 12 jioni. Kwao, ulimwengu mpya ni mwepesi. Unahitaji mengi, pengine. Lakini pia unatoa mengi.
Wengine Wanapambana Kimya Kimya
Kisha wapo ambao hawajawahi kupata mpangilio. Wanazurura, wanachelewa kuamka, hujihisi vibaya, hukimbizana, kisha hupoteza mwelekeo. Wanakosa kubadilishana mawazo ofisini, kurekebishwa na hata vikwazo vidogo vidogo. Bila kujua, husahau jinsi ya kupumzika. Nyumba zao hubadilika kuwa ofisi, na akili zao hazipumziki.

Huenda wasiseme wazi, lakini wamechoka. Sio kutokana na kazi nyingi bali kutokana na kutokujua wakati sahihi wa kupumzika. Hakuna kumaliza kazi ni kila wakati kupokea kazi mpya na kujaribu kuimaliza.
Inabadilisha Hisia Kwenye Timu Pia
Bila chumba, bila meza ya pamoja ofisini au mazungumzo ya koridoni, timu huanza kuhisi tofauti. Watu hugeuka kuwa vyeo vyao, Ukimya unakua kitu cha kawaida. Na utamaduni wa kazini hauji tena, lazima uundwe wakati mwingine kwa aibu, wakati mwingine kwa uzuri, lakini kwa makusudi.
Hakuna muda wa kujuliana hali. Hakuna njia rahisi ya kujua nani ana matatizo au anaendelea vizuri. Inahitaji juhudi Zaidi na Kuuliza zaidi. Wakati mwingine watu hupotea tu kwa muda, na hakuna anayejua hali yao halisi.
Lakini Kuna Ukweli Fulani Ndani Yake
Hata kwa mapungufu yote, mfumo huu mpya una uwazi. Unaonyesha jinsi watu wanavyotegemea ratiba au kutoihitaji sana. Unaonyesha kuwa baadhi walifanya kazi kwa sababu walikuwa wakitazamwa na wengine hufanya vizuri zaidi wanapokuwa peke yao.
Ofisi, kama ilivyokuwa zamani, ilitoa mpangilio fika kazini, fanya kazi za kutosha, na wewe ni sehemu ya malengo makubwa ya ofisi. Sasa, hadithi ni tofauti Wewe mwenyewe unaweka muundo, Wewe unaamua kama siku umeitumia vizuri au sivyo na kufanya hili Si rahisi. Lakini huenda ikawa ni njia ya kweli Zaidi kuwa na utendaji mzuri.