Export Credit Financial Services inawawezesha wasafirishaji wa kitanzania kupitia ujumuishaji wa kifedha

Kibu Logistics Company ni miongoni mwa taasisi zilizopata mtaji kutoka Export Credit Financial Services.
Katika mazingira ya kiuchumi yanayokuwa kwa kasi nchini, moja ya changamoto kubwa inayowakabili wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi hasa biashara ndogo na za kati (SMEs) ni upatikanaji mdogo wa fedha.
Iwe ni mkulima, msafirishaji ama mwagizaji wa bidhaa kutoka nje, changamoto inabakia ile ile, jinsi ya kupata mtaji wa kuzalisha na kusafirisha bidhaa kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
Katika mazingira kama haya, suluhisho pekee la kusaidia kuimarisha uuzaji wa bidhaa nje ni Export Credit Financial Services (ECFS), taasisi ya huduma ndogo za kifedha ambayo imekuwa mhimili mkubwa katika kubadilisha changamoto hii kuwa fursa.
ECFS ni taasisi yenye mikakati imara ya kuhakikisha inafungua fursa za masoko ya kimataifa pamoja na ujumuishaji wa kifedha kwa Watanzania wanaosafirisha bidhaa nje.
Kipi kinaifanya ECFS kuwa tofauti?
Tofauti na benki za kawaida, ECFS inafanya kazi kwa dhamira inayolenga kuondoa pengo lililopo la upatikanaji wa huduma za usaidizi kifedha kwa wasafirishaji bidhaa nje ambao bado hawajafikiwa na huduma hizo. Kama taasisi ndogo ya kifedha, ECFS inatoa suluhu za kifedha kwa biashara ambazo hazipewi kipaumbele na taasisi za mikopo ya kibiashara.
Bidhaa zinazotolewa na ECFS ni; mikopo ya mitaji kwa wasafirishaji bidhaa nje ili kusaidia kukuza shughuli zao za uzalishaji, fedha za kabla na baada ya usafirishaji ili kusaidia kudhibiti vyema mzunguko wa fedha, mikopo ya bima za kusafirisha bidhaa nje ili kulinda bidhaa dhidi ya changamoto za malipo ya wanunuzi wa nje, dhamana ya biashara kwa wafanyabiashara wa ndani na huduma za ushauri wa kifedha kwa SMEs.
Kusaidia ufikiaji wa soko la ndani
Wazalishaji wengi wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto za kufikia hata soko la ndani kutokana na ukosefu wa fedha. ECFS inashughulikia hili kwa kutoa mikopo midogo na bidhaa ambazo zinawawezesha wafanyabiashara kufikia masoko ya kikanda kabla ya yale ya kimataifa.
Kuhamasisha biashara ya kimataifa
ECFS inasaidia kufadhili mauzo ya nje yaliyothibitishwa kwa njia ya punguzo, punguzo la LC na dhamana ya biashara, kuwezesha Barua za Malipo (LCs) kwa kushirikiana na benki za ndani na kimataifa na kutoa bima za malipo katika bidhaa zinazosafirishwa kwenda kwenye nchi za nje kama vile; Uarabuni, Uingereza, Marekani na masoko mengine yote dunian ya kibiashara. Ulinzi huu wa kifedha unawaruhusu wafanyabiashara wa Kitanzania kuingia katika masoko mapya ya kimataifa.
Faida za ECFS kwenye soko la Tanzanian
Upatikanaji wa mitaji nafuu. Kupitia mikopo midogo yenye riba nafuu iliyobuniwa kwa ajili ya wasafirishaji wa bidhaa nje, ECFS inawezesha wafanyabiashara wadogo na vyama vya ushirika kufanya kazi kwa ujasiri.
Ukuzaji wa mauzo ya nje kwa SMEs. Kupitia ECFS, SMEs wanaweza kupata huduma za kifedha ambazo huwaruhusu kutimiza kandarasi kubwa za mauzo ya nje ambapo hapo awali hawakuwa na uwezo huo.
Ujumuishaji wa kifedha. Kwa kuwalenga wafanyabisahara ambazo hawajafikiwa na huduma za kibenki, ECFS inasaidia kuleta biashara nyingi zaidi za Kitanzania katika uchumi rasmi wa kuuza nje.
Uzalishaji wa ajira na ustahimilivu wa kiuchumi. Wauzaji bidhaa nje wanavyokua, wanatengeneza ajira zaidi na kuchangia katika kuimarika kwa uchumi kupitia ongezeko la mapato ya fedha za kigeni.
Kupunguza hatari. Bidhaa za bima za ECFS hulinda wauzaji bidhaa nje dhidi ya changamoto za wanunuzi wa kimataifa, kubadilika kwa thamani ya sarafu na hatari za kijiografia na kisiasa.
ECFS kuleta zama mpya katika usafirishaji nchini
Serikali ya Tanzania imeweka kipaumbele katika ujenzi wa viwanda, uongezaji thamani wa kilimo na maendeleo ya SME. ECFS inalingana kikamilifu na malengo haya ya kitaifa kwa kuhakikisha kuwa fedha si kikwazo tena cha kufikia mafanikio ya mauzo ya nje.
Wakati nchi inatekeleza Dira ya Maendeleo ya 2025-2030 na kuelekea kwenye hadhi ya kipato cha kati, ECFS inaleta mageuzi kwa kuchanganya kanuni za mikopo midogo na uwezeshaji wa biashara ya kimataifa ili kuwawezesha wajasiriamali wa Tanzania.
Export Credit Financial Services
Haidery Plaza, First floor Posta City Center,
Dar es Salaam Tanzania, East Africa
Tel +255 (02)221 13860