Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benki ya CRDB yapata faida Sh206 bilioni robo ya kwanza 2026, yaongoza nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Abdulmajid Mussa Nsekela.

Dar es Salaam. Tarehe 29 Aprili 2026: Baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 206 baada ya kodi katika robo ya kwanza mwaka huu, Benki ya CRDB imeongoza kwa kupata faida kubwa kati ya benki zote za biashara nchini.

Faida hiyo ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 18.9 ikilinganishwa na iliyopata katika kipindi kama hicho mwaka jana, imepatikana baada ya Benki ya CRDB kufanya vyema katika viashiria vyote muhimu vinavyopima mwenendo wa utendaji wa taasisi za fedha ikiwemo faida, ukubwa wa mali, amana za wateja na ufanisi wa uendeshaji.

Akizungumzia matokeo hayo bora zaidi katika historia yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema yanadhihirisha utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano (Evolve Strategy 2023–2027).

“Tulilenga kupata mafanikio haya ndani ya miaka mitano na kweli, tukiwa katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa mkakati wetu wa miaka mitano tumefanikiwa kuwa benki kubwa zaidi nchini na benki inayopata faida kubwa zaidi. Si bahati mbaya bali utekelezaji wa mipango yetu ya ndani,” amesema Dkt. Nsekela.

Mkurugenzi amesema matokeo haya yanaonyesha jinsi Benki ya CRDB ilivyopiga hatua za ukuaji kwa kufanya vizuri katika viashiria vyote vya upimaji mwenendo bora wa kifedha ikiwemo faida, jambo linaloifanya ikose mpinzani katika sekta ya benki nchini.

Kwenye matokeo hayo ya utendaji wa mizi itatu ya kwanza kwa mwaka 2026, faida baada ya kodi imeongezeka kwa asilimia 18.9 hali inayoonyesha ni matokeo ya maamuzi ya kimkakati yaliyohusisha uwekezaji katika sekta zenye tija, kupanua huduma za kidijitali na kudumisha nidhamu katika usimamizi wa mtaji sambamba na kuchochea ukuaji jumuishi wa uchumi.

Ukuaji wa mizania ya benki nao ni miongoni mwa vipimo vilivyoiweka Benki ya CRDB katika nafasi iliyopo sasa. Mali za benki zimeongezeka na kufika shilingi trilioni23.9 huku amana za wateja zikipanda kwa asilimia 9.0 hadi shilingi trilioni 16.3 hali inayoakisi imani thabiti na isiyotetereka kutoka kwa wateja binafsi, kampuni na taasisi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Profesa Neema Mori.

Msingi huu imara wa kifedha umeiwezesha benki kuendelea kukuza mikopo inayotoa ambayo mpaka mwishoni mwa Machi 2026 imefika shilingi trilioni14.7, yakielekezwa zaidi katika sekta muhimu zinazochochea shughuli za kiuchumi.

Wakati huohuo, Benki iliendelea na udhibiti wa vihatarishi ambapo uwiano wa mikopo chechefu umepungua hadi asilimia 2.85. Hii inayoonyesha ukuaji wa uwezo wa benki katika kutoa mikopo huku ikiimarisha mali zake, hali inayosaidia kuifanya biashara hiyo ishamiri katika mazingira yote.

Kwa upande wa mapato, Benki ya CRDB imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa na vyanzo mseto vya mapato kwani yale yatokanayo na riba yaliongezeka hadi kufika shilingi 388.8 bilioni yakichochewa na ukuaji wa mikopo na ongezeko la mapato kutoka kwenye mali zinazozalisha riba.

Sambamba na hilo, Benki imeendelea kuimarisha mapato yasiyotokana na riba, yakichangiwa na ongezeko la miamala kupitia huduma za kidijitali, huduma za benki kupitia mawakala na mifumo ya malipo. Kadri wateja wanavyozidi kutumia huduma za kidijitali, Benki ya CRDB inaendelea kuongeza mapato yatokanayo na miamala huku ikiboresha uzoefu wa wateja, jambo linaloonyesha nguvu ya mfumo wake wa kibiashara unaotegemea majukwaa ya kidijitali.

Mapato ya uendeshaji yaliongezeka hadi shilingi  bilioni 297.6 kutoka shilingi bilioni 254.2 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita, hali inayoonyesha kuwa mageuzi ya kidijitali sasa yamejikita kikamilifu katika shughuli kuu za Benki na hayatazamwi kama fedha za miradi ya pembeni.

Licha ya kuendelea kuwekeza kimkakati katika teknolojia, ikiwemo maboresho ya mfumo mkuu wa uendeshaji pamoja na upanuzi wa shughuli zake kimataifa kupitia ufunguzi wa ofisi ya uwakilishi Dubai, Benki ya CRDB imeendelea kudumisha nidhamu katika matumizi yake. Uwiano wa gharama za uendeshaji dhidi ya mapato ulibaki kuwa asilimia 41.6, ukionyesha uwezo wa benki hiyo kukua kwa ufanisi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori anasema kuwa ufanisi ni nguzo muhimu na taasisi hiyo inatamani kuendelea kubaki kinara wa sekta ya benki nchini.

“Uongozi wetu haupimwi tu kwa ukuaji bali kwa ufanisi wa ukuaji huo. Kuimarisha uwiano wa gharama za uendeshaji dhidi ya mapato wa asilimia 41.6 huku tukipanua shughuli zetu, kunaonyesha uimara wa mfumo wetu wa uendeshaji. Tunaendelea kuhakikisha kuwa ukuaji wa mapato unatafsiriwa kuwa faida endelevu,” anasema Profesa Mori.

Matokeo haya pia yameleta tabasamu kwenye nyuso za wanahisa ambapo faida inayotokana na uwekezaji wa mtaji wa wanahisa ilifikia asilimia 28.0, huku mtaji wa wanahisa ukiongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 3.06. Hii inaendelea kuimarisha nafasi ya Benki ya CRDB kama taasisi yenye mwenendo mzuri wa kiutendaji na yenye uwezo wa kusaidia ukuaji endelevu wa sekta nzima na kuleta maboresho ya muda mrefu. 

Akisisitiza kuhusu mkakati wake, Dkt. Nsekela anasema wakiangalia kule wanakoelekea, anaiona Benki ya CRDB inayoimarisha zaidi uongozi wake sokoni kwa kuharakisha ukuaji katika sekta zenye mchango mkubwa kiuchumi, kupanua mfumo wake wa kidijitali na kutanua wigo wa huduma zake barani Afrika.

“Kwa sasa, hatupambanii kushika usukani wa soko, kwa kuwa tayari sisi ni viongozi. Kipaumbele chetu ni kujiimarisha hapa tulipo kwa kuendelea kubuni na kutoa thamani ya muda mrefu kwa wateja wetu, uchumi na wanahisa. Kwa sasa, Benki ya CRDB ndiyo kiongozi asiye na mpinzani sokoni,” alihitimisha Dkt. Nsekela.