Miili ya watu sita kati ya wanane waliopoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari la wagonjwa (ambulensi) na pikipiki ya miguu mitatu (Guta) imeagwa jana Aprili 21, 2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Upendo, iliyoko katika Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.