Viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama wameshiriki Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi hao alikuwepo Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Mjane wa Hayati Karume, Mama Futuma Karume, Watoto ya Hayati Karume, Amani Abedi Karume na Balozi, Ali Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM (Bara), Stephen Wasira.