Dar es Salaam. Serikali imeendelea kuboresha sekta ya ulinzi na usalama kwa kujenga nyumba 6,064 kwa wanajeshi na kuongeza vifaa na mafunzo ya kisasa. Kwa JKT, idadi ya vijana waliopata mafunzo imeongezeka kutoka 160,427 mwaka 2020 hadi 190,059 mwaka 2025 kupitia miradi ya SUMA JKT. Polisi wamepata ajira 16,000, vyeo 10,363 na vituo 472 vimejengwa hadi ngazi ya kata.
Magereza mapya nane yamejengwa, hospitali ya Dodoma na kutumia TEHAMA katika magereza 66. Zimamoto imepata magari 12, vituo vipya vitatu na boti mbili za uwekezaji. Uhamiaji umeongeza ajira 2,251 huku vita dhidi ya dawa za kulevya ikiimarishwa.