Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Jumatatu, Aprili 7, 2025, ameshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 53 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, yaliyofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandua, Zanzibar.
Viongozi wengine walioshiriki maadhimisho hayo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira, mjane wa hayati Karume, mama Futuma Karume, watoto wa hayati Karume, Amani Abedi Karume na Balozi Ali Abeid Karume, pamoja na Rais mstaafu wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.