Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ushirikiano wa Tanzania na Japan umezidi kuimarika siku ha siku katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia ambapo mauzo ya biashara kati ya nchi hizo yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni saba mwaka 2023 hadi bilioni 37 kwa mwaka 2024.
Majaliwa ameyasema hayo leo Jumapili, Mei 25, 2025 alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World Expo Osaka 2025) yanayoendelea nchini Japan.