Bajeti ya mwaka 2025/26 imelenga kuendeleza na kukamilisha utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo zinazoendana na vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa. Maeneo haya ni pamoja na kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kukuza uzalishaji wa viwanda na huduma, na kuongeza uwekezaji na biashara.