Serikali ya Tanzania imekamilisha na kuzindua Daraja la John Pombe Magufuli, Juni 19, 2025. Daraja hilo refu zaidi Afrika Mashariki na Kati linaunganisha Kigongo-Busisi, likirahisisha usafiri na kufungua fursa za kiuchumi pamoja na kuondoa adha ya vivuko vilivyokuwa vikichelewesha wasafiri.