Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha ambapo anatarajia kufungua Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), leo Jumatano, Juni 4, 2025.