Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zambia yaichimba mkwara Morocco

Kocha wa Zambia, Avram Grant

Muktasari:

  • Zambia ambayo imewahi kutwaa ubingwa huu mara moja imetoka sare mbili, dhidi DR Congo kwenye mechi ya kwanza kabla ya kupata tena matokeo kama hayo kwenye mchezo wa pili dhidi ya Tanzania.

Kocha wa Zambia, Avram Grant amesema timu yake ipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa Kundi F, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Laurent Pokou, San-Pedro, kesho.

Zambia ambayo imewahi kutwaa ubingwa huu mara moja imetoka sare mbili, dhidi DR Congo kwenye mechi ya kwanza kabla ya kupata tena matokeo kama hayo kwenye mchezo wa pili dhidi ya Tanzania.

Zambia kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo baada ya kukusanya pointi mbili, hivyo itahitaji kupata matokeo chanya ili kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora.

Morocco wao baada ya ushindi wa mabao 3-0 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Tanzania, ilifuatia na sare ya bao 1-1 na DR Congo, hivyo hata yenyewe itahitaji matokeo chanya, ili kujihakikishia nafasi nzuri kwenye 16 bora ya fainali hizo za Afcon 2023.

Zambia haitakuwa na huduma ya beki wake, Roderick Kabwe anayetumikia adhabu ya kadi, wakati Kelvin Kapumbu anaweza kuanza baada ya kuonyesha kiwango kizuri mbele ya Tanzania.

“Tunafahamu Morocco ni timu kubwa, lakini hatuwaogopi. Tutacheza nao na natumaini tutaonyesha kiwango bora. Tutawaonyesha uwezo wetu,” amesema Avram Grant kocha wa Zambia.

Wachezaji wa kuchungwa kwenye mchezo huu kwa upande wa Zambia ni Patson Daka, aliyezima ndoto za Tanzania kupata ushindi  wa kwanza kwenye Afcon 2023 baada ya kusawazisha dakika za mwisho na huenda akaendeleza makali yake mbele ya Morocco, ambao silaha yao kubwa na ya kuchungwa ni Youssef En-Nesyri, ambaye amekuwa na kiwango bora.

Morocco na Zambia zipo kwenye kundi moja na timu za DR Congo na Tanzania na zote zitacheza mechi zao za mwisho za hatua ya makundi usiku wa leo Januaru 23, 2024 huku kila moja ikiwa na nafasi ya kupenya hatua inayofuata ya mtoano kwenye 16 bora.

Rekodi zinaonyesha Zambia na Morocco zimekutana mara 18. Simba wa Milima ya Atlas ikishinda mara 10 na Chipolopolo mara sita na mechi mbili zilimalizika kwa sare.