Afcon 2023 inavyoamsha mzuka wa kupiga pesa zaidi

Kipute cha mashindano makubwa na ghali zaidi barani Afrika -- Afcon 2023 – kinatarajiwa kutimka kuanzia Januari 13, 2024. Afrika inasubiri!Tanzania nayo inasubiri! Dunia inasubiri!
Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu, linafanyika kule Ivory Coast na Tanzania ni miongoni mwa mataifa 32 yaliyopata tiketi ya kushiriki katika mashindano hayo ikiwa ni mara ya pili mfululizo ndani ya miaka mitatau kufanya hivyo baada ya miaka zaidi ya 30 kupita.
Homa na shauku ya mashindano inazidi kupanda kwa wadau wa michezo barani kote kutokana na kuongezeka kwa ubora kwa baadhi ya mataifa katika soka, matumizi ya teknolojia saidizi za uamuzi kama vile VAR, ushindani wa timu za madaraja ya kati, msimamo wa makundi na zawadi zinazowaniwa katika mashindano hayo.
Wakati hayo yanaendelea, mtandao maarufu wa utabiri wa matukio makubwa ya michezo, Opta, umetoa ubashiri wake kwa timu zinazoweza kuchukua ubingwa wa mwaka huu, huku zile tano za juu ni pamoja na Senegal ikiongoza kwa asilimia 12.8, Ivory Coast (12.1), Morocco (11.1), Algeria (9.7), Misri (8.5).
Hizi zinaweza kuwa si taarifa za kushtua wala kuzua taharuki kwa wapenda soka barani Afrika lakini ni taarifa nyeti kwa wazee wa mikeka kupitia SportPesa. Hakuna mtu anayesubiri kwa hamu kuanza kwa michuano hii kama watandika jamvi.
Opta imewarahisishia kazi wabashiri wa michezo kupitia Sportpesa kuanza kujiandaa kuchagua odds zenye uhakika wa matokeo mazuri na kushinda fedha lukuki.
We ingia katika tovuti ya www.sportpesa.co.tz au pakua programu tumishi yako ya Sportpesa App jisajili na usubiri kipute kianze, utanishukuru.