Yanga yatawala tuzo Ligi Kuu

Muktasari:
- Dube ameibuka mchezaji bora wa mwezi akiwashinda kiungo wa timu yake, Stephanie Aziz KI na mshambuliaji wa KenGold, Selemani Bwenzi.
Mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube na kocha wake, Miloud Hamdi wamebeba tuzo za ubora za Ligi Kuu Bara mwezi Februari.
Dube ameibuka mchezaji bora wa mwezi akiwashinda kiungo wa timu yake, Stephanie Aziz KI na mshambuliaji wa KenGold, Selemani Bwenzi.
Ndani ya Februari, Dube, raia wa Zimbabwe alikuwa wa moto ambapo kwenye mechi saba alizotumia dakika 562 alifunga mabao matano na kutoa asisti tano akihusika kwenye jumla ya mabao 10.
Wakati Dube akitamba hivyo, Hamdi amebeba tuzo yake ya kwanza ya kocha bora akiwashinda Fadlu Davids wa Simba na Fred Minziro wa Pamba Jiji aliochuana nao.
Hamdi aliiongoza Yanga kushinda mechi nne za ligi akiifanya Yanga kukusanya pointi 12.
Ndani ya mechi hizo walizifunga KMC, Singida Black Stars, Mashujaa na Pamba Jiji - Yanga ikifunga jmabao 16 huku ikiruhusu mawili.