Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yajiwahi mapema CAF, Kamwe atoa angalizo

Muktasari:

  • Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza ugenini huko Angola dhidi ya Wiliete na ikisonga raundi ya pili itakutana na mshindi baina ya Silver Strikers ya Malawi dhidi ya Elgeco Plus ya Madagascar.

Yanga imesikia adhabu ambayo watani wao wa jadi, Simba wamepewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) , wakaamua kupeana tahadhari mapema siku moja kabla ya mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete, kesho Jumamosi, Septemba 27, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mashabiki na wanachama wa Yanga wametahadhalishana kuwa wale watakaokuwepo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuhakikisha hawafanyi vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu au vile vitakavyokiuka kanuni za ulinzi na usalama ili nao wasipigwe rungu na CAF.

Kupitia taarifa ambayo Umoja wa Matawi ya Yanga umeisambaza katika makundi ya mtandao wa Whatsapp, mashabiki wa timu hiyo wamesisitizwa kutoiweka klabu matatani.

"Tarifa hii ipelekeni kwenye matawi yote na magroup yote ya Yanga. Jumamosi hii timu yetu ya Yanga inacheza mechi ya marudiano na  hawa ndugu zetu wa Angola. Hii mechi sisi Yanga ndio wenyeji

"Kuna taratibu za CAF ambazo tusipozifuata tutaiingiza klabu yetu kwenye matatizo ya kupigwa faini. Kama tunavyofahamu faini za CAF ni kubwa hivyo tunawaomba sana  wanachama wetu wapenzi wetu na mashabiki wetu Jumamosi tujiepushe na hivi vitu ambavyo vinaweza kuingiza klabu yetu kwenye hasara ya kupigwa faini.

"Kuwasha Ile mioshi, kupiga mafataki, kubeba bendera au mabango  yanayoashiria siasa na. kuonyesha picha za wanasiasa tunapokua uwanjani. Hivyo ni vitu ambayo CAF wanavikataza na tukiviruhusu kuingia uwanjani tutaisababishia klabu yetu kuwa kwenye matatizo," inafafanua taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesisitiza mashabiki kufanyia kazi kile ambacho wameshauriwa.

"Tumeshaongea na vijana wetu wa ulinzi kuhakikisha wanafanya ukaguzi milangoni wakati mashabiki wanaingia na kuhakikisha wanavizuia vitu vyote vitakavyoiletea  hasara klabu yetu.

"Tunaomba ushirikiano kutoka kwa kila atakaekuja kusapoti timu yetu jumamosi. Wenzetu wamezuiliwa kuingiza mashabiki timu yao inapocheza hivyo nasi tuwe makini tusije tukaingia kwenye mtego huo. Kila mmoja awe mlizi wa mwenzake uwanjani. Tuzuie kwa pamoja viashiria vyovyote vinavyoweza kuingiza klabu yetu kwenye matatizo," umeendelea kufafanua ujumbe huo.

Hilo linajitokeza wakati ambao CAF im epiga Simba faini ya Dola 85,000 kwa makosa ya mashabiki wake katika mechi mbili za Kombe la Shirikisho Afrika nyumbani dhidi ya Al Masry katika robo fainali na dhidi ya RS Berkane katika fainali.

Wakati mashabiki wa Yanga wakipeana angalizo hilo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe amesema matokeo ya mchezo wa kwanza ambao walishinda ugenini hayapaswi kuwafanya wajione wameshafuzu raundi ya pili hivyo mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu kesho.

"Mchezo wetu wamarudiano hatupaswi kubweteka kutokana na matokeo yaliyopita. Bila shaka mmewasikia wapinzani wetu wakisema kuwa bado wana imani ya kubadilisha matokeo. Kocha wa timu pinzani bado anayo matumaini makubwa.

"Huu ni mpira wa miguu tunapaswa kuwa makini sana. Mashabiki wetu tunawaomba wajiitokeze kwa wingi kuwapa vijana hamasa," amesema Kamwe.