Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaitamani Simba, kuendeleza ubabe

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 7, 2024 kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii. Picha na Yanga

Muktasari:

  • Yanga imetamba kuwa wamejipanga kwa ajili ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1:00 usiku.

Dar es Salaam. Benchi la ufundi na wachezaji wa Yanga wametamba kuwa wamejipanga kuendeleza ubabe wao dhidi ya Simba kwa kuibuka na ushindi katika mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa licha ya kutopata nafasi ya kuitazama vya kutosha Simba, haimpi presha kwa vile kikosi chake kina ubora wa hali ya juu.

Gamondi amesema kuwa amejikita zaidi katika kuifanya Yanga iwe bora uwanjani katika mechi hiyo akiamini hiyo ni silaha kubwa ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

“Hakuna siri kwenye mpira kila kitu lazima kiwe hadharani. Kesho ni siku muhimu sana kwani ni mechi ya mtoano. hatupaswi kufanya makosa tunapaswa kuwa makini kwenye kila idara ili kupata matokeo mazuri, naamini mashabiki wetu watajitokeza kwa wingi kwa lengo la kutupa hamasa.”

“Naheshimu sana wapinzani wote ninaokutana nao. Kesho ni mchezo wa dabi hakuna 'underdog' (timu isiyopewa nafasi) kwenye mchezo huo kwani ni mchezo maalumu sana. Najua mpinzani wetu ana timu mpya, wachezaji wapya, wote kwa pamoja watachukua fursa hii kuonesha ubora wao.

Aidha kocha huyo amesema kimsingi mchezo huu mizani ipo sawa kwa pande zote 50/50 huku akisisitizi kwenda kwa umakini mkubwa kwenye mechi hiyo.

"Tupo imara kiakili na kimwili. Tumejianda vya kutosha hakuna tunachohofia. Sijapata wasaa mzuri wa kuwatazama wapinzani kwani mechi zake nyingi hazikuoneshwa, lakini hiyo sio changamoto kubwa kwani naanda timu yangu kwa asilimia 75, asilimia 25 ndio natumia kumchunguza mpinzani," amesema Gamondi.

Kipa wa Yanga, Abubakar Khomein amesema kwa upande wao wachezaji wapo tayari kwa mechi hiyo.

“Tumejiandaa vizuri sana na tuko tayari, wachezaji wana ari na wote tunawahakikishia kuwa wachezaji tunakwenda kupambana, naamini kesho tutafanya vizuri," amesema Khomein.

Mshindi wa mechi hiyo ya Yanga dhidi ya Simba kesho atakutana na mshindi wa mechi baina ya Azam na Coastal Union ambao utachezwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni.

Fainali ya Ngao ya Jamii itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Agosti 11.

Msimu uliopita Simba ilitwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Yanga katika fainali kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa suluhu.