Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yafungiwa kusajili

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji kwa kosa la kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano, Cliford Mario Ndimbo inasema "Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo."
"Pamoja na masuala mengine, Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS) licha ya kukumbushwa kufanya hivyo."
"Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza  matakwa hayo ya kikanuni na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikisha kwa ajili ya hatua zaidi.

"Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF nalo limefungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani."
Yanga inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Fountain Gate kesho Aprili 12 katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.