Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaaga Ligi ya Mabingwa Afrika

Muktasari:

  • Yanga imefuzu mara moja tu katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu muundo wa mashindano hayo ulipobadilika 2004.

Dar es Salaam. Yanga imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kulazimishwa sare tasa na MC Alger kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Matokeo hayo yameifanya Yanga imalize katika nafasi ya tatu kwenye kundi A ikiwa na pointi nane nyuma ya vinara Al Hilal yenye pointi 10 na MC Alger yenye pointi tisa katika nafasi ya pili.

Licha ya kutawala mchezo wa kwa muda mwingi, Yanga ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata na kujikuta ikimaliza dakika 90 bila bao, matokeo ambayo yamekuwa na faida kwa wapinzani wao.

Pamoja na kocha Sead Ramovic kufanya mabadiliko mawili kwenye mechi ya jana, mambo hayakuenda sawa kwa timu yake hadi filimbi ya kumaliza mchezo ilipopulizwa.

Kocha huyo aliwatoa Kennedy Musonda, Mudathir Yahya na kuwaingiza Pacome Zouzoua na Clatous Chama huku wapinzani wao wakiwatoa Larbi Tabti, Akram Bouras, Tayeb Meziani, Amine Messoussa na Soufiane Bayazid ambao nafasi zao zilichukuliwa na Zakaria Naidji, Andy Delort, Hamza Mouali, Abdelkader Menezia na Zakaria Draoui.

Katika mechi hiyo, refa Patrice Milazare kutoka Mauritius aliwaonyesha kadi za njano, Abdelatif Ramdane, Ayoub Ghezala na Mohamed Halaimia kwa sababu tofauti ambazo ni kupoteza muda na kucheza rafu.

Kwa kushindwa kutinga robo fainali, Yanga inakosa kiasi cha Dola 900,000 (Sh2.3 bilioni) ambacho kila timu inayotinga hatua hiyo inajihakikishia kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Yanga kwa kuishia hatua ya makundi, itaondoka na kifuta jasho cha Dola 700,000 (Sh1.8 bilioni) kutoka CAF.

Msimu uliopita, Yanga iliishia hatua ya robo fainali ambapo ilitolewa kwa mikwaju ya penalti 3-2 na Mamelodi Sundowns baada ya mechi mbili baina yao kumalizika kwa sare tasa.