Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga watua TPLB na wanasheria watatu kisa dabi

Dar es Salaam. Viongozi wa Klabu ya Yanga wamefika rasmi katika ofisi za Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kwa ajili ya kikao kilichoitishwa na uongozi wa bodi hiyo, huku msafara wao ukiwa na viongozi watano na wanasheria watatu.

Msafara huo uliwasili majira ya saa 4:12 asubuhi, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Arafat Haji. Wengine waliokuwepo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai na Rodgers Gumbo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo.

Pia walikuwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe, sambamba na jopo la wanasheria watatu wa timu hiyo.

Akizungumza kwa kifupi mara baada ya kuwasili, Arafat amesema: "Tumefika na muungwana hakatai wito," kabla ya kuingia ndani ya ofisi za TPLB kwa ajili ya mazungumzo yaliyopangwa kufanyika leo.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.