Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

White arudishwa England, majeraha yakimzuia Eze

Beki wa Arsenal, Ben White ameitwa na meneja Thomas Tuchel kuchukua nafasi ya Jarell Quansah ambaye ameumia. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Ben White ameichezea timu ya Taifa ya England katika mechi nne na mechi yake ya mwisho ilikuwa ni Machi 20222 dhidi ya Ivory Coast.


Baada ya kukaa nje ya kikosi cha England tangu alipokuwemo mara ya mwisho katika Fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatar, beki wa Arsenal, Ben White leo, Jumatatu, Machi 23, 2026 amejumuishwa kundini.

White ameitwa na meneja Thomas Tuchel kuchukua nafasi ya Jarell Quansah ambaye ameumia kabla timu hiyo haijacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uruguay na Machi 27 na Machi 31 mwaka huu.

Beki huyo wa kulia alijiondoa katika kambi ya England wakati wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, siku moja baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wales.

Inaripotiwa kwamba Ben White alipishana kauli na Mwneja Msaidizi, Steve Holland na akaamua kuondoka huku akisisitiza hatorejea tena.

Baadaye iliripotiwa kwamba ugomvi baina ya Ben na Holland uliibuka baada ya meneja huyo msaidizi kuhoji maslahi ya White kwa mchezo wa soka.

Majadiliano baina yao inaripotiwa yalifanyika mbele ya wachezaji wengine wa England jambo lililomkwaza White na kuamua kujiondoa kikosini.

Machi 2024 Ben White aliweka msimamo wake kuwa hatokuwa tayari kucheza timu ya Taifa ya England hadi pale ambapo ingeachana na Gareth Southgate.

Hata hivyo Januari mwaka huu, Southgate alifungishwa virago na nafasi yake imechukuliwa na Thomas Tuchel ambaye ameamua kumrudisha kundini White.

Wakati Ben White akiitwa katika timu ya taifa ya England, nyota wa Arsenal Eberechi Eze amejiengua kikosini.

Eze amejiweka kando baada ya kupata majeraha ya kigimbi cha mguu.