Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu atoa maagizo mawili Uwanja wa AFCON Arusha

Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo mkoani Arusha leo Aprili 17, 2026 ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya AFCON 2027.

Muktasari:

  • Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa AFCON Arusha ulianza Machi 2024 ukitarajiwa kuingiza mashabiki 30,000 na kutumika kwa fainali za AFCON 2027 zitakazofanyika Tanzania, Kenya na Uganda.

Arusha. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba leo, Ijumaa, Aprili 17, 2026, ametoa maagizo mawili kwa wanaosimamia mradi wa ujenzi wa Uwanja wa soka wa Arusha utakaotumika kwa Fainali za AFCON 2027.

Maagizo hayo ni uharakishwaji wa mradi huo pamoja na matumizi stahiki ya fedha za ujenzi wa uwanja huo.

Amesema uwanja huo unatakiwa kukamilika mapema ili kuendana na muda wa maandalizi waliopewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

“Kaguzi zitakuja mapema zaidi ya hapa. Fanyeni kazi usiku na mchana. Tusiweke dosari ambazo hazihusiani na maandalizi ya viwanja. Ongezeni vitendea kazi, ongezeni nguvu kazi ili tutekeleze mapema huo muda ambao tumeuweka.

“La pili tuendelee kuzingatia thamani na viwango vya fedha. Tutimize mahitaji na matakwa ya waendesha shughuli wa AFCON lakini lazima tuwape thamani ya viwango Watanzania ambao ndio watoa fedha ya ujenzi,” amesema Mwigulu.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Uwanja huo jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema kuwa Uwanja huo utakuwa na vitu vingi vya kuufanya uwe miongoni mwa viwanja bora Afrika.

Utakuwa miongoni mwa viwanja vitatu bora barani Afrika vinavyoonyesha uhalisia wa maisha na jiografia ya Afrika. Viwanja vyetu vingi tulivyonavyo havina sehemu ya watu mashuhuri. Mtu kama Rais ni kiongozi mkubwa. Uwanja huu umemtambua na kumpa nafasi yake.

“Kuna vyumba 15 maalum vya VIP ambavyo tutavitoa kwa kuvipa majina ya viongozi wetu waliofanya kazi iliyotukuka katika nchi hii ya Tanzania.

“Mzee wetu Molinge Edward Sokoine lazima jina lake liwepo mahala pale kama sehemu ya watu waliojenga kumbukumbu katika mkoa wetu wa Arusha,” amesema Makonda.