Prime
Wagombea waanza kulia uchaguzi TFF

Muktasari:
- TFF ilitangaza tarehe ya kuchukua fomu ilikuwa Juni 16 hadi Juni 20 jioni ambapo kwa nafasi ya urais fomu inagharimu shilingi 500,000, huku Kamati ya Utendaji ikiwa 200,000.
Wakati mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF ukiendelea, wagombea wameanza kulia na baadhi ya hatua katika kufanikisha kurudisha fomu za nafasi za juu.
Kilio hicho kimetolewa na mgombea wa nafasi ya Urais Injinia Mustapha Himba akisema mara baada ya kuchukua fomu hiyo, amekumbana na kigingi kigumu kuidhinishwa na wajumbe wa uchaguzi huo.
Akizungumza na vyombo vya habari jana, Himba alisema mara baada ya kuchukua fomu hizo, amepambana kutafuta wajumbe lakini wameshindwa kumpa ushirikiano akijibiwa tayari uidhinishwaji huo umeshafanyika kwa mmoja wa mgombea mmoja ambaye hata hivyo, hakumtaja.
"Kugombea ni haki ya kila anayejiona ana sifa na nilipojipima nikaona natosha na kwenda kuchukua fomu, wote mliona kwenye huu uchaguzi kuna wagombea wa nafasi ya rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji," alisema Himba.
"Mimi nilijipima na kutaka kugombea nafasi ya rais, lakini kwenye Ile fomu kuna eneo linanitaka nipate uidhinishwaji wa angalau wajumbe watano, nimezunguka sana naambiwa watu 46 kati ya 47 walishampa mgombea mmoja.
"Sasa unajiuliza mchakato umeanza jana tu leo watu 46 waliwezaje kumuidhinisha huyu mtu mmoja tena wengine wakisema mengi zaidi.
"Tungeambiwa mapema tu kwamba uchaguzi huu una mgombea mmoja tu wa nafasi ya rais tusingehangaika kuchukua fomu na tumelipa fedha kwa hiyo hiki kwangu hakipo sawa na natafuta haki yangu.
"Nampongeza rais aliye madarakani Wallace Karia amefanya mengi mazuri lakini nadhani alipaswa kutoa nafasi ili watu tumpime kama yale mazuri aliyoyafanya yakamsaidie kwa wapiga kura, watoe nafasi ya wengine kumpa changamoto, nataka kwenda kumsaidia."
TFF ilitangaza tarehe ya kuchukua fomu ilikuwa Juni 16 hadi Juni 20 jioni ambapo kwa nafasi ya urais fomu inagharimu shilingi 500,000, huku Kamati ya Utendaji ikiwa 200,000.
Naye Mwanasheria wa mgombea huyo Wakili msomi Aloyce Komba alisema :"Haoni kama kila kitu kinaweza kufanyika siku mbili, hivyo kama kuna namna imefanyika basi ni jinai, vyombo husika vinatakiwa kuchunguza hilo ili watu wote wapate haki, kama watu wameitwa kuchukua fomu inakuaje akose wadhamini ambao ni wajumbe, sasa pesa za watu zisiende bure.
"Tukienda katika kanuni za TFF, zinazungumziaje udhamini, kanuni za uchaguzi za mwaka 2021 ,Ibara ya 10(3)