Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wababe uwanjani England

Muktasari:

  • Tottenham itakipiga na Tamworth, timu inayoshika daraja la chini zaidi kwenye michuano hiyo na itakuwa ugenini. Wakati huo, Coventry City iliyocheza nusu fainali msimu uliopita itakuwa nyumbani kuwakaribisha Sheffield Wednesday.

LONDON, ENGLAND. Mabingwa watetezi wa Kombe la FA, Manchester United itakipiga na Arsenal baada ya vigogo hao wa Ligi Kuu England kupangwa kumenyana kwenye mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA baada ya droo iliyofanyika usiku wa juzi Jumatatu.

Katika droo hiyo, wakati Man United ikiwa na kasheshe la kwenda kuikabili Arsenal uwanjani Emirates, Aston Villa wao watakuwa Villa Park kukipiga na West Ham United katika vipute viwili vinavyohusisha timu zote za Ligi Kuu England katika raundi hiyo.

Kwingineko, Manchester City itacheza na Salford City katika dabi ya mtaani. Salford City ni timu inayomiliwa na wachezaji wa zamani wa Man United, akiwamo Gary Neville. Chelsea itacheza na Morecambe inayoshika mkia kwenye League Two, wakati Accrington Stanley itaifuata Liverpool huko uwanjani Anfield.

Tottenham itakipiga na Tamworth, timu inayoshika daraja la chini zaidi kwenye michuano hiyo na itakuwa ugenini. Wakati huo, Coventry City iliyocheza nusu fainali msimu uliopita itakuwa nyumbani kuwakaribisha Sheffield Wednesday.

Mechi zote zitachezwa wikiendi ya Januari 11, 2025.

Washindi 32 wa raundi ya tatu watavuna Pauni 115,000, wakati timu zitakazopoteza kwenye raundi hiyo zitalipwa Pauni 25,000. Na mechi zote zitachezwa siku moja, huku marudiano yakifutwa na kuongeza dakika za ziada na pengine penalti kama kutakosekana mshindi kwenye muda wa kawaida wa mchezo. Man United na Arsenal ndiyo timu zenye historia nzuri zaidi kwenye Kombe la FA na miamba hiyo imeshinda ubingwa wa taji hilo mara 13 na 14 mtawalia. Kipute kingine kitashuhudia Southampton ikicheza na Swansea huko St Mary's, huku kukiwa na London derby na Millwall itacheza na Dagenham & Redbridge, wakati timu ya Wayne Rooney, Plymouth Argyle itacheza na Brentford, Newcastle itakipiga na Bromley, Bristol na Norwich.

Kali zaidi, baba na mwana watakutana kwenye raundi hiyo, wakati Ashley Young na kikosi chake cha Everton kupangwa kumenyana na Peterborough United, timu anayochezea mwanaye wa miaka 18, Tyler.