Liverpool inautaka Ubingwa EPL

Muktasari:
- Mara ya mwisho Liverpool ilichukua taji la EPL msimu wa 2019/2020 ambapo katika mechi 13 ilishinda mechi 12 na kutoa sare moja huku ikikusanya pointi 37 ilipokuwa chini ya kocha Jurgen Klopp ambaye ameondoka msimu uliopita.
Liverpool imezidi kujiweka pazuri kwenye kilele cha Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Anfield.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Cody Gakpo dakika ya 12 akipewa pasi na Mohamed Salah huku bao lingine likifungwa dakika ya 78 na Mohamed Salah kwa mkwaju wa penalti ambapo amefikisha michezo 36 aliyofunga na kutoa pasi iliozaa bao.
Kocha wa Liverpool Arne Slot mpaka sasa ameiongoza timu hiyo kushinda mechi 11 katika michezo 13 ya Ligi ambapo amepata sare moja na kupoteza mechi moja huku akiwa ameshinda michezo 17 katika mashindano yote aliyoiongoza Liverpool.
Mara ya mwisho Liverpool ilichukua taji la EPL msimu wa 2019/2020 ambapo katika mechi 13 ilishinda mechi 12 na kutoa sare moja huku ikikusanya pointi 37 ilipokuwa chini ya kocha Jurgen Klopp ambaye ameondoka msimu uliopita.
Manchester City chini ya Guardiola inaendelea kufanya vibaya ikiwa imeruhusu vipigo vinne kwenye Ligi Kuu ya England ambapo imeshuka mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 23 kwenye mechi 13 ilizocheza huku ikiruhusu mabao 19 kati ya 22 iliofunga.
Uwanja wa Anfield umekuwa mgumu kwa Pep Guardiola ambapo kwenye michezo 10 alioiongoza Man City amefanikiwa kupata ushindi mara moja, sare tatu na kupoteza mechi sita huku mara ya mwisho City ilishinda mabao 4-1 mwaka 2021.
Liverpool imefikisha pointi 34 ikiwa inaongoza kwenye msimamo wa EPL ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 25 ikiwa nafasi ya pili sawa na Chelsea yenye pointi 25 ikiwa nafasi ya tatu ambapo nafasi ya nne inashikwa na Brighton yenye pointi 23.
Matokeo ya mechi nyingine
Chelsea 3 -0 Aston Villa
Man United 4 - 0 Everton
Tottenham 1 - 1 Fulham
West Ham 2 - 5 Arsenal
Brentford 4 - 1 Leicester
Crystal Palace 1 -1 Newcastel
Nottingham 1 -0 Ipswich
Wolves 2 -4 Bournemouth
Brighton 1 - 1 Southampton