Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya ubingwa Yanga, Simba inavyosubiri majibu ya mwisho

Muktasari:

  • Yanga inahitaji matokeo ya ushindi tu katika mechi ya mwisho dhidi ya JKT Tanzania ili iweze kutwaa ubingwa.

Dar es Salaam. Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu, atapatikana katika raundi ya mwisho, Jumanne, Juni 30, 2026 baada ya Yanga na Simba kila moja kupata ushindi katika mechi yake leo.

Matokeo hayo yameifanya Yanga iendelee kuongoza msimamo wa Ligi ikifikisha pointi 72 huku Simba ikifikisha pointi 70 na kuendelea kubaki katika nafasi ya pili.

Kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, wenyeji Yanga wameibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United, yote yakipachikwa na Allan Okello.

Mabao hayo yamemfanya Okello afikishe idadi ya mabao 14 moja pungufu dhidi ya Feisal Salum ambaye yuko kileleni mwa chati ya kuwania Ufungaji Bora wa msimu.

Pia Okello anakuwa mchezaji wa nne kufunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi moja, wengine wakiwa ni Mossi Nduwumwe (Singida BS), Mathew Tegis (Pamba Jiji) na Fabrice Ngoy (Namungo FC).

Simba imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars.

Mabao ya Simba katika mchezo wa leo yamefungwa na Elie Mpanzu na Anicet Oura.

Katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amejitengenezea mazingira mazuri ya kuibuka Mfungaji Bora wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kupachika bao katika ushindi wa mabao 2-0 ambao Azam FC iliupata dhidi ya wenyeji Coastal Union, ambapo bao lingine lilifungwa na Landry Zouzou.

Fei Toto anaendelea kuongoza orodha ya wafungaji bora wa ligi akifuatiwa na Okello na Mossi Nduwumwe wa Singida Black Stars wakiwa na mabao 14.


Matokeo ya mechi za leo

Yanga 3-0 TRA United

Simba 2-0 Singida BS

Coastal 0-2 Azam FC

Namungo 0-0 Fountain Gate

Dodoma Jiji 1-1 Mbeya City

Pamba Jiji 1-2 JKT Tanzania

Mashujaa FC 2-0 KMC

Tanzania Prisons 2-1 Mtibwa Sugar