Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Nistelrooy ameanza alipoishia

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyu wa zamani wa Manchester United alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Leicester City mwishoni mwa mwezi Novemba akichukua mikoba ya Steve Cooper ambaye alionekana kufanya vibaya kwa mabingwa hawa wa mwaka 2016.

Kocha mpya wa Leicester City Ruud Van Nestelrooy ameanza vyema kibarua kipya hapo jana baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa King Power.

Leicester ilipata bao la kwanza dakika ya pili ambalo lilifungwa na Jamie Vardy kabla ya Decordova-Reid kufunga bao la pili dakika ya 81 ambapo bao la tatu lilifungwa dakika ya 90 na Patson Daka raia wa Zambia huku bao la kufutia machozi la West Ham lilifungwa dakika za nyongeza na Niclas Füllkrug.

Van Nistelrooy ameendelea pale alipoishia baada ya kuondoka Man United akiwa hajapoteza mchezo wowote alipokuwa kocha wa muda ambapo alicheza mechi tatu za Ligi huku akishinda mechi mbili na kupata sare mechi moja.

Kwenye michezo hiyo mitatu aliyoiongoza United, mmoja kati ya miwili aliyoshinda aliifunga Leicester City mabao 3-0 akifanya hivyo mara mbili baada ya kuifunga kwenye Kombe la Carabao mabao 5-2 akiwa ndiyo kocha wa kwanza kuifunga timu mechi mbili na baadae kuiongoza kama kocha ndani ya msimu mmoja kwenye EPL.

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Manchester United alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Leicester City mwishoni mwa mwezi Novemba akichukua mikoba ya Steve Cooper ambaye alionekana kufanya vibaya kwa mabingwa hawa wa mwaka 2016.

Baada ya ushindi wa jana Leicester imesogea mpaka nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 13 nyuma ya West Ham ambayo inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 15 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 14.

West Ham imefungwa mara mbili mfululizo baada ya kutoka kupoteza mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Arsenal ilipokubali kipigo cha mabao 5-2 wakati Leicester imepata ushindi wa kwanza tangu Oktoba 19, 2024 iliposhinda mabao 3-2 ugenini dhidi ya Southampton.

Mchezo mwingine uliopigwa jana ulikuwa kati ya Ipswich Town ambayo ilikubali kipigo cha bao 1-0 ikiwa nyumbani dhidi ya Crystal Palace. Ipswich Town imefungwa mechi saba, imetoa sare mechi sita huku ikiwa imeshinda mechi moja kwenye michezo 14 iliocheza ambapo inashika nafasi ya 19 ikiwa na pointi tisa mbele ya Southampton inayobuluza mkia ikiwa na pointi tano.

Michezo mingine ya Ligi kuu England ‘EPL’ itaendelea tena leo kwenye viwanja sita tofauti ambapo Pep Guardiola baada ya kupoteza mechi nne za Ligi ataiongoza Man City itakayokuwa nyumbani dhidi ya Nottingham Forest huku mechi kubwa zaidi itakuwa kati ya Arsenal itakayokuwa nyumbani dhidi ya Manchester United.


Ratiba ya michezo ya leo EPL

Arsenal vs Manchester United

Aston Villa vs Brentford

Everton vs Wolverhampton

Manchester City vs Nottingham Forest

Newcastle United vs Liverpool

Southampton vs Chelsea