Ushindi wa jioni ulivyompa rekodi Amorim United

Muktasari:
- Ruben Amorim ameweka rekodi ya kuipa ushindi United ikiwa kwenye aridhi ya Jamuhuri ya watu wa Czech, tangu mwaka 2004 ilipopata sare ya 0-0 dhidi ya Sparta Prague.
Manchester United imefanikiwa kupata ushindi hapo jana baada ya kuifunga Viktoria Plzen mabao 2-1 kwenye mchezo wa Europa uliopigwa Uwanja wa Doosan Aréna.
Ushindi wa jana unaifanya United kufikisha michezo sita bila kupoteza ambapo imepata sare michezo mitatu na kupata ushindi michezo mitatu huku kocha Ruben Amorim akiweka rekodi ya kuipa ushindi United ikiwa kwenye aridhi ya Jamuhuri ya watu wa Czech, tangu mwaka 2004 ilipopata sare ya 0-0 dhidi ya Sparta Prague.
Ruben Amorim amefanikiwa kuifikia rekodi ya kuiongoza timu kucheza michezo sita bila kupoteza tangu alipofanya hivyo David Moyes alipokuwa akiiongoza Manchester United msimu wa 2013-2014.
Mabao ya United yalifungwa na Rasmus Højlund dakika ya 62 ambapo alisawazisha bao la Viktoria Plzen lililofungwa dakika ya 48 na Matěj Vydra, ambapo bao la ushindi lilifungwa dakika ya 88 na Højlund tena.
Mabingwa hawa wa Europa mwaka 2017 wamesogea mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 12. kinara ni Lazio mwenye pointi 16 sawa na Athletic Club inayoshika nafasi ya pili, wakati nafasi ya tatu inashikwa na Anderlecht ikiwa na pointi 14 huku Lyon na Eintracht Frankfurt zikishika nafasi ya nne na tano zikiwa na pointi 13.
Man United imebakiza mechi mbili kwenye mashindano haya ambapo Januari 23, 2025 itacheza dhidi ya Rangers kwenye Uwanja wa Old Trafford kabla ya kwenda Romania kuvaana na Steaua București, huku ikipewa nafasi ya kumaliza nane bora.
Matokeo ya mechi nyingine
Roma 3-0 Braga
Viktoria Plzeň 1-2 Manchester United
Malmö 2-2 Galatasaray
Olympiacos 0-0 Twente
PAOK 5-0 Ferencváros
Ludogorets 2-2 AZ Alkmaar
Union SG 2-1 Nice
Hoffenheim 0-0 FCSB
Ajax 1-3 Lazio
Porto 2-0 Midtjylland
Bodø/Glimt 2-1 Beşiktaş
Elfsborg 1-0 Qarabağ
Maccabi Tel-Aviv 2-1 RFS
Lyon 3-2 Eintracht Frankfurt
Rangers 1-1 Tottenham Hotspur
Real Sociedad 3-0 Dynamo Kyiv
Slavia Praha 1-2 Anderlecht