Chelsea inavyofaidi upana wa Kikosi

Muktasari:
- Chelsea ilipata ushindi huku wachezaji kama Noni Madueke, Enzo Fernandez, Jadon Sancho na Nicolas Jackson wote wakibaki England, wakati Cole Palmer mfungaji wao bora katika Ligi Kuu ya England, akiwa hayumo katika kikosi cha Europa Conference.
Chelsea imeendelea kuonyesha ubora wake baada ya kupata ushindi wa tano mfululizo ikiifunga Astana mabao 3-1 ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Ortalyq katika michuano ya Europa Conference.
Licha ya kupumzisha wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kocha wa Chelsea Enzo Maresca alifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mabingwa hao wa Kazakhstani ambao wamekuwa na wakati mgumu katika mashindano haya ambapo wanashika nafasi ya 28 wakiwa wameshinda mechi moja, sare moja, huku wakipoteza mechi tatu kati ya tano walizocheza.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Marc Guiu dakika ya 14 akifunga bao la kwanza kabla ya kufunga bao lingine dakika ya 19 huku Renato Veiga akifunga bao la tatu dakika ya 40 ambapo bao la kufuta machozi la Astana lilifungwa dakika ya 45 kabla ya mapumziko kwa shuti kali lililopigwa na nahodha Marin Tomasov.
Wachezaji wa kikosi cha pili pamoja na wale waliyopangwa kutoka kituo cha kukuzia vipaji cha Cobham ambao walicheza mechi yao ya kwanza kwenye mashindano ya Ulaya walipambana na kuonyesha mchezo mzuri ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Wachezaji kama Noni Madueke, Enzo Fernandez, Jadon Sancho na Nicolas Jackson wote walibaki England, huku Cole Palmer mfungaji wao bora katika Ligi Kuu ya England, akiwa hayumo katika kikosi cha Europa Conference.
Hali hiyo ilimfanya Marc Guiu, mwenye umri wa miaka 18, kuongoza safu ya ushambuliaji, huku Sam Rak-Sakyi (19), Josh Acheampong (18) na Tyrique George (18) wakianza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza katika historia ya Chelsea kuanza na wachezaji wanne wa umri mdogo katika mashindano ya Ulaya.
Kuanzishwa kwa Shim Mheuka kulimfanya kuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo zaidi kucheza kwenye mashindano ya Ulaya akiwa na miaka 17 na siku 54 baada ya Dominic Solanke kuwahi kufanya hivyo alipokuwa Chelsea.
Rak-Sakyi alionyesha utulivu na umahiri akiwa na mpira, bila shaka alionyesha kiwango bora kwenye eneo la kati ambapo wamekuwa wakicheza Moises Caicedo na Romeo Lavia.
Kikosi cha Chelsea dhidi ya Astana
Golipa: Filip Jorgensen
Mabeki: Joshua Acheampong, Tosin Adarabioyo, Axel Disasi, Renato Veiga
Viungo: Rak-Sakyi, Dewsbury-Hall, Carney Chukwuemeka
Washambuliaji: Pedro Neto, Marc Guiu, Tyrique George
Matokeo ya mechi nyingine
Astana 1-3 Chelsea
Fiorentina 7-0 LASK
Copenhagen 2-0 Hearts
Dinamo-Minsk 2-0 Larne
Noah 1-3 APOEL
Petrocub 0-1 Real Betis
HJK Helsinki 2-2 Molde
İstanbul Başakşehir 3-1 Heidenheim
Legia Warszawa 1-2 Lugano
Olimpija Ljubljana 1-4 Cercle Brugge
St. Gallen 1-4 Vitória SC
Mladá Boleslav 1-0 Jagiellonia Białystok
Gent 3-0 TSC
Omonoia 3-1 Rapid Wien
Pafos 2-0 Celje
Shamrock Rovers 3-0 Borac
The New Saints 0-2 Panathinaikos
Víkingur Reykjavík 1-2 Djurgården