Juventus ilivyoitibulia Man City usiku wa Ulaya

Muktasari:
- Mabingwa hawa wa mwaka 2023 wamebakiza michezo miwili kukamilisha idadi ya michezo nane ambapo Januari 22, 2025 watakuwa wageni wa PSG kabla ya kumaliza na Club Brugge kwenye Uwanja wa Etihad, Januari 29, 2025.
Manchester City imeendelea kufanya vibaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 hapo jana dhidi ya Juventus kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa kwenye Uwanja wa Allianz, Torno, Italia.
Mabao ya Juventus yalifungwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila mshindi ambapo dakika ya 52 Dusan Vlahovic aliipatia Juventus bao la kwanza kabla ya Mckannie kufunga lingine dakika ya 75 ambalo lilidumu mpaka dakika 90 zinamalizika.
Baada ya kipigo cha jana dhidi ya Juventus, Man City imeshuka mpaka nafasi ya 22 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa na pointi nane wakati Juventus imepanda mpaka nafasi ya 14 ikiwa na pointi 11 katika michezo sita.
Mabao mawili waliyofungwa Man City yanaifanya kuruhusu mabao mengi katika mashindano yote iliyocheza kuliko timu nyingine za ligi tano bora Ulaya ambapo Man City mpaka sasa imeruhusu mabao 21 katika michezo nane.
Mabingwa hawa wa mwaka 2023 wamebakiza michezo miwili kukamilisha idadi ya michezo nane ambapo Januari 22, 2025 watakuwa wageni wa PSG kabla ya kumaliza na Club Brugge kwenye Uwanja wa Etihad, Januari 29, 2025.
Michezo mingine iliyochezwa usiku wa jana ilishuhudiwa Arsenal ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Monaco ambapo mabao ya Arsenal yalifungwa na Bukayo Saka aliyefunga mawili dakika ya 34 na dakika ya 78 wakati bao la tatu lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 88.
Baada ya ushindi wa Arsenal dhidi ya Monaco unaifanya kufikisha michezo 14 bila kufungwa ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani ambapo imeshinda michezo 12 huku ikipata sare michezo miwili kwenye dimba la Emirates.
Matokeo ya mechi nyingine
Atlético Madrid 3-1 Slovan Bratislava
LOSC Lille 3-2 Sturm Graz
AC Milan 2-1 Crvena Zvezda
Arsenal 3-0 Monaco
Borussia Dortmund 2-3 Barcelona
Feyenoord 4-2 Sparta Praha
Juventus 2-0 Manchester City
Benfica 0-0 Bologna
Stuttgart 5-1 Young Boys