Amorim kufukuzia rekodi leo

Muktasari:
- Mara ya mwisho United ilicheza dhidi ya Sparta Prague mwaka 2004 ambapo mchezo ulimalizika kwa sare ya 0-0 huku ikisubiriwa leo kama wataweza kupata ushindi wa kwanza wakiwa nchini humo.
Meneja wa Man United Ruben Amorim huwenda akaweka rekodi ya kuiongoza United kupata ushindi kwenye aridhi ya Jamuhuri ya watu wa Czech dhidi ya Viktoria Plzen katika mchezo wa Ligi ya Europa.
Mara ya mwisho United ilicheza dhidi ya Sparta Prague mwaka 2004 ambapo mchezo ulimalizika kwa sare ya 0-0 huku ikisubiriwa leo kama wataweza kupata ushindi wa kwanza wakiwa nchini humo.
United inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kutoka kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu England ambapo ilipoteza mabao 2-0 dhidi ya Arsenal huku ikipoteza mabao 3-2 ikiwa nyumbani dhidi ya Nottingham Forest, Desemba 8, 2024.
Manchester inashika nafasi ya 12, ikiwa na pointi tisa kwenye michezo mitano iliyocheza sawa na Viktoria Plzen ambayo inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi tisa huku United ikiizidi tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ikiwa imefunga mabao 10 ikiruhusu mabao saba wakati Viktoria Plzen imefunga mabao tisa ikiruhusu mabao saba.
Iwapo leo, United itapata matokeo mazuri itafikisha michezo sita bila kupoteza kwenye mashindano haya ambapo Ruben Amorim atakuwa kocha wa kwanza kuongoza mechi sita za mashindano ya Ulaya bila kupoteza tangu alipofanya hivyo David Moyes akiwa na Manchester United msimu wa 2013-2014.
Mechi nyingine za Leo
AS Roma vs Braga
Viktoria Plzen vs Manchester United
Malmö FF vs Galatasaray
Olympiacos vs FC Twente
PAOK vs Ferencvaros
Ludogorets Razgrad vs AZ Alkmaa
Union Saint-Gilloise vs Nice
TSG Hoffenheim vs FCSB
Ajax vs Lazio
FC Porto vs FC Midtjylland
FCSB vs Olympiacos
Bodo/Glimt vs Besiktas
IF Elfsborg vs FK Qarabag
Maccabi Tel-Aviv vs Rigas Futbola Skola
Lyon vs Eintracht Frankfurt
Rangers FC vs Tottenham Hotspur
Real Sociedad vs Dynamo Kyiv
Slavia Prague vs Anderlech