Ugumu Simba, JKT Tanzania huu hapa

Muktasari:
Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 34 na JKT Tanzania inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 19.
Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola na kocha mkuu wa JKT Tanzania, Ahmad Ally wamefichua kile ambacho kitafanya mechi baina ya timu hizo kesho kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kuwa ngumu.
Matola alisema kuwa kutofanya vizuri kwa JKT Tanzania kutafanya wacheze mechi ya kesho kwa juhudi kubwa ili wavune pointi tatu zitakazofanya wasogee juu katika msimamo wa ligi.
“Haitakuwa mechi rahisi. JKT Tanzania ni miongoni mwa timu nzuri na bora zaidi kwenye ligi. Ukichukulia kwamba wamekuwa hawana matokeo mazuri katika mechi lakini wamekuwa na kiwango bora sana.
“Pamoja na ugumu wao, tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mechi ya kesho. Tumekuwa tunapata matokeo lakini tumekuwa tukiruhusu magoli.
“Sisi kama benchi la ufundi hatufurahishwi na mwenendo huo na tumekuwa tukilifanyia kazi nina imani taratibu na kuanzia mechi ya kesho tutajitahidi kuweza kurekebisha hilo na lisiweze kujitokeza tena,” alisema Matola.
Kocha wa JKT, Ahmad Ally alisema wanahitajika kuwa na kiwango bora zaidi ili waibuke na ushindi dhidi ya Simba
“Maandalizi yako vizuri. Kitu kikubwa ambacho nafikiri tunaweza kuwa tumejiandaa nacho sana ni kiakili. Kama mwalimu, kitu kikubwa ambacho nakiona tunaweza kukiandaa sana ni akili ya kujua jinsi gani tunaweza kujipanga uwanjani tukiwa na mpira na tukiwa hatuna mpira.
“Tunajua tunakwenda kucheza na timu bora kwa sasa kwenye nchi yetu na kipindi cha nyuma huko na unaweza kuona jinsi gani wako bora kwenye kila nyakati na wanaweza kupata matokeo nyumbani na ugenini hivyo mwalimu Fadlu na benchi lake wamefanya kazi kubwa,” alisema Ally.
Mchezo huo wa Simba na JKT Tanzania, awali ulikuwa uchezwe Oktoba 29, 2024 lakini uliahirishwa hadi kesho, Desemba 24, 2024 baada ya JKT Tanzania kupata ajali ya gari ilipokuwa ikitokea Dodoma kucheza na Dodoma Jij