Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuachane na Uwanja, tuwaze mechi-Ahmed Ally

Muktasari:

  • Simba ilitinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Berkane, Morocco. Uongozi wa Simba licha ya kupata kigugumizi kujibu suala la mabadiliko ya uwanja wa mechi yake ya marudiano ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenda Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar umewataka mashabiki wake kuwa na utulivu na kuelekeza akili katika mechi ya kwanza ambayo itachezwa keshokutwa Jumamosi jijini Berkane Morocco.

Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kwa sasa uongozi unajikita na mchezo wa kwanza wa fainali dhidi ya Berkane ambao utachezwa Mei 17, 2025 katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane na baada ya hapo utatoa taarifa rasmi kuhusu hatima ya mechi ya marudiano nyumbani.

"Tumepokea taarifa hiyo na maelekezo ambayo nimeelekezwa na viongozi wangu niwamabie ninyi wanadishi wa habari na Wanasimba kwa ujumla ya kwamba kwa sasa uongozi wa klabu ya Simba umejikita kwenye maandalizi ya mechi ya tarehe 17.

"Fikra,maandalizi, mipango na kila kitu tumekielekeza katika mechi yetu ya keshokutwa. Taarifa rasmi kuhusiana na mechi yetu ya tarehe 25 zitatolewa punde baada ya mechi yetu ya tarehe 17. Tukishamaliza mchezo huo tutakuja kuwaambia mustakabali wa mechi yetu ya tarehe 25.

"Lakini kwa sasa Wanasimba waendelee na maandalizi ya taarifa ya awali. wale wa mikoani waendelee na mpango wakuja Dar es Salaam hadi pale tutakapotoa taarifa nyingine ambayo itakuwa rasmi," amesema Ahmed.

Hata hivyo habari za uhakika ni kwamba mchezo huo utachezwa visiwani Zanzibar katika Uwanja wa New Amaan Complex na tayari Simba, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na serikali tayari wameshajulishwa mabadiliko hayo ya ratiba na CAF.

Hii ni mara ya pili kwa mechi ya Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimuhuu kuchezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya mashindao hayo baina ya Simba ns Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Jean Charles Ahoua ambalo liliiwezesha kuifanya ifuzu hatua ya fainali ya mashindano hayo.


Wachezaji wasema jambo

Nyota wa Simba wamewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi na mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco, Jumamosi, Mei 17, 2025 katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.

Wachezani hao Shomari Kapombe, Che Fondoh Malone na Kibu Denis wamesema kuwa wapo katika maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi hiyo na hata ya marudiano.