Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Steve Barker kocha mpya Simba

Muktasari:

  • Steve Barker aliiongoza Stellenbosch kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Dar es Salaam. Simba leo Ijumaa, Desemba 19, 2025 imemtangaza Steve Barker kutoka Afrika Kusini kuwa Kocha Mkuu mpya.

Barker (57), anajiunga na Simba akitokea Stellenbosch aliyoiongoza kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Katika msimu huu, Barker ambaye alizaliwa nchini Lesotho, ameiongoza Stellenbosch katika michezo 24 ya mashindano tofauti.

Timu hiyo katika mechi hizo 24, imepata ushindi mara nane, kutoka sare sita na kupoteza mechi 10.

Kabla ya kuiongoza Stellenbosch, Barker alizifundisha pia Mpumalanga Black Aces, Amazulu na Chuo Kikuu cha Pretoria.

Ni kocha anayeheshimika sana kwa mchango wake katika kukuza vipaji vya vijana na ujenzi wa timu zenye nidhamu na mtindo wa kisasa wa kucheza.

Barker anachukua mikoba iliyoachwa wazi na Dimitar Pantev ambaye Simba iliachana baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Mechi hizo ni dhidi ya Petro Luanda ambayo Simba ilifungwa bao 1-0 nyumbani na dhidi ya Stade Malien ambayo Simba ilifungwa mabao 2-1 ugenini.

Kocha huyo anakuwa wa tatu kuifundisha Simba msimu huu baada ya Fadlu Davids na Pantev.