Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot, Van Dijk waweka rekodi Liverpool ikitwaa Ubingwa

Muktasari:

  • Arne Slot amekuwa kocha wa kwanza kutoka Uholanzi kutwaa taji la EPL huku Van Dijk akifanya hivyo akiwa kama nahodha wa timu hiyo.

Luverpool, England. Baada ya kuiongoza Liverpool kushinda taji la Ligi Kuu England (EPL) ambapo ilitangaza ubingwa huo katika mchezo dhidi ya Tottenham uliochezwa Jumapili, Aprili, 27 ilipopata ushindi wa mabao 5-1 kwenye uwanja wa Anfield.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot pamoja na nahodha wa timu hiyo Virgil van Dijk wameweka rekodi baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda taji hilo la EPL.

Arne Slot ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutokea taifa la Uholanzi kushinda taji la Ligi Kuu England akiwashinda Louis van Gaal na Erik ten Hag ambao waliwahi kupita kwenye Ligi hiyo bila kutwaa ubingwa.

Katika Ligi Kuu ya England msimu huu walikuwepo makocha watatu kutokea Uholanzi ambao ni Erik ten Hag aliyekuwa Man United kabla ya kufungashiwa vilago na mwingine ni Ruud van Nistelrooy ambaye alitimkia Leicester City iliyoshuka daraja.

Slot mwenye umri wa miaka 46 pia ameingia kwenye rekodi ya kuwa miongoni mwa makocha watano waliofanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England katika msimu wa kwanza akiungana na Jose Mourinho (Chelsea) msimu 2004-2005, Antonio Conte (Chelsea) msimu 2016-2017, Carlo Ancelotti (Chelsea) msimu 2009-2010 na Manuel Pellegrini (Manchester City) msimu 2013-2014.

Mbali na Arne Slot, Virgil van Dijk pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Uholanzi kushinda taji la EPL akiwa kama nahodha akifanya hivyo msimu huu baada ya kuondoka kwa Jordan Henderson aliyekuwa naodha wa timu hiyo.

Mwingine ni Dominik Szoboszlai ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka taifa la Hungary kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England. Szoboszlai amechangia kuisaidia Liverpool akiwa amehusika katika mabao 10 akifunga matano na kutoa asisti tano.

Liverpool imefikisha jumla ya mataji 20 ya Ligi Kuu England sawa na Manchester United iliyokuwa ikiongoza kwa mataji mengi ya EPL hapo kabla. Mara ya mwisho Liverpool ilitwaa taji hilo msimu wa 2019-2020 ikiwa imepita miaka mitano hadi wamekuja kufanya hivyo tena mwaka huu.