Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot amkumbuka Salah akikiri pengo lake

Muktasari:

  • Salah ameifungia Misri mabao manne katika Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2025 huku akifunga idadi kama hiyo ya Mabao katika Ligi Kuu England.

London, England. Meneja wa Liverpool, Arne Slot amesema atafurahi kumpokea tena mshambuliaji Mohamed Salah huku akidokeza kwamba mpasuko uliokuwapo baina yao umekwisha.

Salah anayeitumikia Misri hivi sasa katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 alijikuta katika huzuni juzi Jumatano baada ya timu yake kufungwa bao 1-0 na Senegal kwenye nusu fainali ya mashindano hayo, lililofungwa na nyota mwenzake wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane.

Fainali hizo za AFCON 2025 zinaonekana zimerudisha makali ya Salah katika kufumania nyavu ambapo amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya mwisho jambo linalomkosha Slot ambaye amekiri kwamba anatamani mshambuliaji huyo kurejea klabuni hivi sasa.

“Kwanza kabisa, anahitaji kucheza mechi nyingine kubwa kwa ajili ya Misri Jumamosi (mechi ya kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Nigeria).

“Nina furaha kwamba anarejea. Mo (Salah) amekuwa muhimu sana kwa klabu hii, na pia kwangu, hivyo nina furaha kwamba amerudi.

“Hata kama ningekuwa na washambuliaji 15, bado ningefurahi kama angerudi, lakini hiyo si hali yetu kwa sasa,” amesema Slot.

Haya yanajiri baada ya Slot na Salah kuwa na mgogoro kufuatia mshambuliaji huyo kusema kuwa wawili hao ‘hawana uhusiano’ katika mahojiano yaliyozua mjadala mkubwa, baada ya kukaa benchi la akiba kwa kipindi fulani mwezi Desemba.

Bado haijafahamika ni mchezo gani Salah atarejea kucheza, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 yuko kwenye mazungumzo na Slot kuhusu kama atarejea kwa mechi ya Ligi ya Mabingwa ugenini dhidi ya Marseille Jumatano, au mchezo wa ligi dhidi ya Bournemouth Jumamosi inayofuata.

Salah huenda akahitaji siku chache za kupumzika kabla ya kurejea majukumu ya Liverpool  baada ya kumalizika kwa fainali za AFCON 2025, ingawa kwa sasa anaweza kuhitajika zaidi kutokana na wimbi la majeruhi, likiwahusisha mshambuliaji Alexander Isak pamoja na mabeki kadhaa ambao watakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.