Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sio siri tena, Xabi Alonso ni mali ya Madrid

Muktasari:

  • Romano alidai kwamba Alonso atakwenda Madrid pamoja na wasaidizi wake na mkataba aliosaini utafika kikomo 2028. Na kwamba ataanza majukumu mapema kabisa ya kuiongoza Real Madrid kwenye Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika huko Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13.

Madrid, Hispania. Anatoka mwanaume, anaingia mwanaume. Ndicho unachoweza kusema baada ya kuripotiwa kocha Xabi Alonso amesaini mkataba wa kuinoa Real Madrid hadi 2028.

Na kwamba ataanza kazi ya kuinoa timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Dunia la klabu. Kocha Ancelotti ataondoka kwenye timu hiyo mwisho wa msimu, kumpisha Alonso kuja kuanzisha zama mpya.

Alonso kwa sasa ni kocha wa klabu ya Bayer Leverkusen, inayoshiriki mikimikiki ya Bundesliga, ambapo msimu uliopita ilibeba ubingwa wa ligi hiyo bila ya kupoteza mechi hata moja.

Mkataba aliosaini huko Bernabeu ni wa miaka mitatu, kwa mujibu wa Fabrizio Romano, ambaye aliposti jambo hilo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X.

Romano alidai kwamba Alonso atakwenda Madrid pamoja na wasaidizi wake na mkataba aliosaini utafika kikomo 2028. Na kwamba ataanza majukumu mapema kabisa ya kuiongoza Real Madrid kwenye Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika huko Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13.

Hata hivyo, Real Madrid bado haijatangaza kuthibitisha hilo, lakini mabosi wa Bayer Leverkusen hawana shida ya kumruhusu kwa upendo wote kocha huyo kwenda kutimiza ndoto za maisha yake.

Alonso alishawahi kuichezea Real Madrid kuanzia 2009 hadi 2014. Baada ya kumalizana na maisha ya soka kama mchezaji, alianza kazi ya ukocha, alianza kuinoa timu ya watoto ya Real Madrid hadi wenye umri wa miaka 14 kabla ya kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa Real Sociedad B.

Na kuanzia 2022 amekuwa kocha mkuu wa  Leverkusen, ambayo ilibeba Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Super Cup ya Ujerumani msimu uliopita, ambapo timu ilimaliza msimu wote bila ya kupoteza mechi kwenye Bundesliga.

Mabosi wa Leverkusen wamebariki kocha huyo kuondoka. Kwa sasa Real Madrid itaendelea kuwa chini ya kocha Ancelotti kumalizia mechi tatu zilizobaki kwenye La Liga. Kocha huyo Mtaliano amekuwa kwenye kikosi cha Los Blancos tangu 2021, ambapo ilikuwa awamu yake ya pili kuinoa timu hiyo.

Katika awamu yake ya pili Real Madrid, Ancelotti ameshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, Klabu Bingwa Dunia, La Liga mara mbili, Copa del Rey na Spanish Super Cup mara mbili.

Taarifa za kutoka Hispania zinafichua kwamba Ancelotti atakwenda kuinoa timu ya taifa ya Brazil.