Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS, Simba hakuna mnyonge 

Dar es Salaam. Singida Black Stars inaialika Simba kwenye Uwanja wa Liti, Singida leo kuanzia saa 10:00 huku kila upande ukiwa hauna sababu ya kutishwa na mwingine huku ukipaswa kuamini unao uwezo wa kushinda mechi.

Timu hizo mbili zina vikosi vyenye wachezaji wengi wenye ubora, muendelezo wa matokeo mazuri na pia ziko juu kwenye msimamo wa ligi, sababu zinazoupa ukubwa mchezo wa leo.

Tangu ilipoanza kuitwa Singida Black Stars, hii ni mara ya kwanza kwake kukabiliana na Simba kwenye Ligi Kuu lakini kabla ya hapo ilikuwa ikiitwa Ihefu na iliwahi kukutana na Simba kwenye ligi mara sita tofauti.

Katika mara hizo sita ambazo timu hizo zimewahi kukutana kwenye ligi wakati huo Singida Black Stars ikiitwa Ihefu, Simba imeibuka na ushindi mara tano na zimetoka sare mara moja.

Timu hizo mbili zinakutana huku Simba ikiwa na muendelezo bora zaidi wa kufanya vizuri kwenye ligi ingawa Singida Black Stars nayo mambo yanaonekana kuiendea vizuri.

Katika mechi tano zilizopita za Ligi, Simba imepata ushindi mara zote huku Singida Black Stars ikipata ushindi mara tatu, kutoka sare moja na kupoteza mechi moja.

Simba ikipata ushindi katika mechi ya leo itafikisha pointi 40 ambazo zitaifanya iendelee kuongoza msimamo wa ligi na Singida Black Stars ikipata ushindi itapanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwani itafikisha pointi 36.

Uwanja wa nyumbani umekuwa silaha ya Singida Black Stars kwani wamepoteza mechi moja tu kwenye ligi kati ya nane walizocheza nyumbani wakishinda mechi tano na kutoka sare mbili.

Simba nayo imekuwa tishio ugenini msimu huu kwani imeshinda mechi zote sita ilizocheza ugenini msimu huu.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids alisema wanafahamu wanacheza na timu imara hivyo wametoa saa vyema kwa ajili ya mechi hiyo.

“Tunajua tunakutana na timu nzuri sana yenye wachezaji wazuri na inayofundishika. Ni timu ambayo inafunga na ina ubora kote katika eneo la kuchezea.  Lakini hatutakiwi kufikiria ni kwa namna gani tunaweza kuwadhibiti kufunga ila tunafikiria zaidi kufunga dhidi yao.

“Hauwezi kuchezesha kikosi kilekile kwenye kila mechi. Ni ngumu kumwambia mchezaji acheze kila mechi na akupe kiwango kilekile. Jambo la muhimu kwetu ni kuhakikisha tunajitahidi kuwa na muendelezo,” alisema Davids.

Kocha wa Singida Black Stars, Ramadhan Nsanzurwimo alisema kuwa wanaamini kucheza nyumbani kutakuwa na faida kwao.

“Utakuwa mchezo mgumu na sisi tumejiandaa kutokana na ubora wa Simba. Tuna ubora kwenye kikosi chetu, tunajua Simba inakuja na maswali ya kutuuliza na sisi tutawajibu na sisi tuna maswali yetu ya kuwauliza. Ni mechi inayohitaji umakini sana.

“Tunaiheshimu Simba lakini hatuiogopi. Kutokana na wachezaji tulionao na timu yetu na tuko nyumbani, tuko na vitu vyote ambavyo tunaweza kutumia ili tushinde vita hii. Pointi tatu itakuwa na umuhimu sana,” alisema Nsanzurwimo.

Ukiondoa mechi hiyo ya Singida Black Stars dhidi ya Simba, mechi nyingine itakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma kuanzia saa 12:15 jioni ambapo Dodoma Jiji FC itaikaribisha Mashujaa FC.