Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penalti ya Ahoua yaiokoa Simba jioniiiiiii

Muktasari:

  • Ahoua amehusika na mabao 11 ya Simba, akifunga mabao saba na kupiga pasi nne za mwisho katika Ligi Kuu.

Bao la mkwaju wa penalti la dakika za lala salama la Charles Ahoua leo limeiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa KMC Complex, lililoifanya timu yake izidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikifikisha pointi 37.

Penalti hiyo ilitolewa na refa Kefa Kayombo kutoka Mbeya baada ya Mohamed Bakari kumfanyia faulo, Shomari Kapombe katika eneo la hatari la timu yake.

Bakari alimvuta na kumuangusha Kapombe aliyekuwa akiiwahi pasi ya Ahoua jambo lililomlazimu refa Kayombo kupuliza filimbi ya kuashiria pigo la penalti na ndipo Ahoua akaukwamisha kimiani na kuifanya timu yake iibuke na ushindi huo.

Mbali na uamuzi huo, refa Kayombo pia alimuonyesha kadi nyekundu, Bakari kwa vile kadi ya njano aliyopata kwa tukio hilo ilikuwa ya pili kwake kwenye mechi ya jana licha ya kuingia akitokea benchi.

Kwa kufunga bao hilo, Ahoua sasa amefikisha idadi ya mabao saba yanayomfanya ashike nafasi ya pili kwenye chati ya kufumania nyavu huku kinara akiwa ni Elvis Rupia ambaye amefumania nyavu mara nane.

Pamoja na kupoteza mchezo huo, JKT Tanzania walicheza vyema katika eneo lao la ulinzi ambapo walizuia hatari nyingi walizoelekezewa na wachezaji wa Simba katika dakika zote za mchezo wakiongozwa na kipa Yakoub Suleiman ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika.

Kocha wa KMC, Ahmad Ałły amesema amefurahishwa na namna wachezaji wake walivyofanyia kazi mpango wa mechi japo wamepoteza.

“Nipongeze wachezaji kwa jinsi ambavyo tulikuwa na mpango. Tulijaribu kuona bora kwenye kila eneo. Simba eneo ambalo wako vizuri ni katikati hivyo tuliamua kuwa imara katikati.

“Ukiwabana katikati watalazimika kupitia pembeni kupitia mabeki wao wa pembeni hivyo sisi tushambulie kwenye nafasi ambazo mabeki wao wa pembeni wataziacha. Sio mbaya tunashukuru kwa hiki kilichotokea japo haikuwa malengo,” alisema Ahmad.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi.

“Pongezi nyingi kwa wachezaji. Tumecheza mechi nne ndani ya muda mfupi. Hongera kwa JKT Tanzania kwa kuweza kucheza vizuri kwa ajili ya kutuzuia. Kungekuwa na penalti nyingine kwa vile kuna mtu alishika ndani ya boksi.

“Zilikuwa ni jitihada kubwa. Wachezaji wamepambana na mwisho wa siku tumeweza kupata ushindi nawapongeza wachezaji,” alisema Fadlu Davids.

Mkoani Singida kwenye Uwanja wa Liti, wenyeji Singda Black Stars waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kengold.

Mabao ya ushindi ya Singida Black Stars yalifungwa na Arthur Bada na Elvis Rupia huku la Kengold likipachikwa na Herbert Lukindo.