Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS, Azam shughuli pevu

Muktasari:

  • Mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo ulinmalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Dar es Salaam. Mechi nne za Ligi Kuu ya NBC zitachezwa leo katika viwanja na miji tofauti nchini lakini gumzo ni mchezo baina ya Singida Black Stars dhidi ya Azam ambao utafanyika katika Uwanja wa Liti, Singida kuanzia saa 10:15 jioni.

Nafasi kwenye msimamo wa ligi na pengo dogo la pointi ambalo lipo baina ya timu hizo linafanya mchezo wa leo uwe wa lazima kushinda kwa mojawapo ili itibue hesabu za nyingine.

Azam inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 51, ushindi katika mechi ya leo utaifanya iwe mbele ya Singida Black Stars kwa tofauti ya pointi saba na hivyo itajiweka katika uwezekano mkubwa wa kumaliza katika nafasi tatu za juu ambazo zitaihakikishia tiketi ya kushiriki mashindano ya klabu Afrika msimu ujao.

Lakini kama Singida Black Stars iliyo nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 itapata ushindi leo, maana yake itakuwa nyuma ya Azam kwa pointi moja na hivyo kuendelea kuipa presha katika mbio za kumaliza katika nafasi tatu za juu.

Katika mchezo wa leo, Azam FC itapaswa kumchunga zaidi mshambuliaji wa Singida Black Stars ambaye ameonyesha uwezo wa hali ya juu wa kufumania nyavu tangu alipojiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la usajili ambapo katika mechi nane alizocheza za Ligi Kuu amefunga mabao nane.

Singida Black Stars nayo hapana shaka itapaswa kumchunga zaidi Djibril Sillah wa Azam FC ambaye hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao nane kwenye ligi.

Katika michezo mitano iliyopita ya Ligi Kuu, Singida Black Stars imepata ushindi mara tatu, imepoteza moja na kutoka sare moja wakati Azam imepata ushindi mara mbili na kutoka sare tatu.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo ulinmalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kocha wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema kuwa timu yake inaingia katika mechi hiyo ikiwa inajiamini.

“Nina imani kwa wachezaji wangu. Tuna timu na tupo imara kiakili. Kila mechi ina mpango wake,” alisema Taoussi.

Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma alisema kuwa wanaiheshimu Azam lakini wanaamini wanaweza kuwafunga.

“Azam ni timu nzuri na wako juu yetu kwenye msimamo wa ligi hivyo tunapaswa kuwa na tahadhari dhidi yao ingawa hatuwahofii kwani na sisi tuna kikosi kziuri,” alisema Ouma.

Katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, Tanzania Prisons itaikaribisha Kagera Sugar, Dodoma Jiji itailika Kengold kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na mchezo mwingine utakuwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Lindi ambao utazikutanisha Namungo na KMC.