Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yapokewa kwa shangwe Dar

Muktasari:

  • Simba imeingia mara mbili katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni 1993 katika Kombe la CAF na mara ya pili ni msimu huu.

Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kimewasili mchana huu kikitokea Zanzibar ambako jana kilicheza mechi ya pili ya marudiano ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Katika mchezo huo, Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yameifanya RS Berkane itwae ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025.

Pamoja na kushindwa kutwaa ubingwa, kikosi cha Simba kimepokelewa kwa shangwe pindi kilipowasili hapa bandarini.

Kikosi hicho kimewasili saa 7:10 mchana kwa boti na baada ya kumaliza taratibu za ukaguzi, kilianza kutoka nje na wachezaji kuingia moja kwa moja kwenye basi la timu hiyo.

Shangwe hizo za mashabiki wa Simba katika mapokezi ya timu hiyo zinaongozwa na mashabiki wa Simba ambao wapo na kikundi chao cha ngoma ambacho kimekuwa kikiambatana na timu hiyo katika maeneo mbalimbali inakocheza.

Nyimbo mbalimbali za kusifu wachezaji na makocha wa timu hiyo zimekuwa zikiimbwa pamoja na viongozi wa Simba kwa kuiwezesha timu hiyo kufika hatua ya fainali.

Shamrashamra hizo za mashabiki wa Simba zimesababisha kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuri hapa bandarini.

Baada ya wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi wote kuingia kwenye basi, msafara wa Simba umeondoka huku ukiendelea kushangiliwa na mashabiki hao ambao  baada ya hapo wametawanyika.

Kwa kufika fainali, licha ya kupoteza, Simba imejihakikishia kitita cha Sh2.7 bilioni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Katika mchezo wa jana, bao la Simba lilifungwa na Joshua Mutale na lile la kusawazisha la RS Berkane lilipachikwa na Soumaila Sidibe.