Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yabadilisha mikakati, yaipeleka Stellenbosch Zenji

ZENJI Pict

Muktasari:

  • Katika hatua ya nusu fainali, Simba itakabiliana na Stellenbosch ya Afrika Kusini ambapo mchezo wa kwanz utachezwa hapa Tanzania, Aprili 20 na mechi ya marudiano itachezwa Afrika Kusini, Aprili 27.

Simba imeamua kuweka kambi ya siku tano visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch kufuatia uamuzi wa kutumia Uwanja wa New Amaan Complex kwa mechi hiyo badala ya Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Baada ya kufahamu rasmi kuwa haitotumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi hiyo ya kwanza nyumbani, Simba imeamua kupunguza siku za kuwepo Dar es Salaam ili ikapate muda mwingi Zanzibar ambako mechi hiyo itachezwa.

ZEN 01

Lengo la kutumia takribani siku tano Zanzibar ni kuzoea eneo la kuchezea la Uwanja wa New Amaan Complex ambao Simba haijautumia kwa mwaka mzima tangu ilipocheza Fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Azam FC, Aprili 27, 2024.

“Pamoja na jitihada za kuuweka sawa Uwanja wa Benjamin. Mkapa, hakuna uwezekano ukawa tayari kwa mechi yetu dhidi ya Stellenbosch na utahitaji siku kama 20 hivi uwe sawa hivyo hauwezi kuwahi tarehe ya mchezo.

ZEN 03

“Muda mfupi ujao tutatangaza rasmi kuutumia Uwanja wa New Amaan Complex kwa mechi yetu dhidi ya Stellenbosch na taratibu zote muhimu tumeshakamilisha.

“Kikosi kitaondoka Dar es Salaam Jumatano au Alhamisi kwenda Zanzibar kwa kambi ya kujiandaa na mchezo huo. Tayari timu ya utangulizi imeshafika Zanzibar kuweka mambo sawa,” kimesema chanzo ndani ya Simba.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa robo fainali baina ya Simba na Al Masry ambao wawakilishi hao wa Tanzania waliibuka na ushindi wa mabao 4-1, serikali ilitangaza kuufungia kwa muda Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatangaza kuufunga uwanja wa Benjamin Mkapa kwa muda kuanzia leo tarehe 9 Aprili 2025 ili kupisha marekebisho ya eneo la kuchezea (Pitch) lililopata athari kubwa kufuatia mvua zilizonyesha na kufuatiwa na mchezo wa Robo Fainali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba SC na Al Masry ya Misri.

“Timu ya Wataalamu itaanza mara moja kufanya tathmini ya kina ya madhara yaliyojitokeza na tarehe ya kufunguliwa kwa uwanja huo itatangazwa hapo baadaye.

ZEN 02

Kufuatia uamuzi huu, timu zote ambazo zilipanga kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa zikiwemo zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa zinaombwa kutafuta uwanja mbadala wakati Serikali ikifanya marekebisho ya eneo la kuchezea kwa dharura.

“Wizara inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na kufungwa kwa uwanja huu kwa sasa,” ilifafanua taarifa ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.